Ualbino sio kosa, tofauti zetu zisitubague

Imeandikwa na Salmin Juma , Zanzibar

Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mgeni Hassan Juma amesema kila mtu anahaki sawa katika nchini iwe ni albino au mtu mwengine, na  serikali haipo tayari kuona mtu anavunjiwa haki zake kwa kisingizio cha hali ya kimaumbile aliyokua nayo.

Kauli hiyo ameitoa leo alipokuwa akizungumza na watu wenye ualbino katika ukumbi wa Uhuru uliyoko katika viwanja cha kufurahishia watoto kariakoo, ambapo leo ni siku maalum ya  uzinduzi wa taasisi All Albinism pamoja  na siku ya Albino duniani (siku ya uwelewa kwa albino) inayoadhimishwa kila June 13 ya kila mwaka.

Akizungumza katika hadhara hiyo Naibu Spika amesema ni lazima kuwa pamoja na watu wenye ualbino kwasababu wanaishi katika mazingira magumu, na ni muhimu sana kuzidishwa elimu kwa wananchi kwani ndio itakayo wafanya wawe kitu kimoja katika kuishi vizuri na albino.

 “hawa ni binaadamu sawa na wengine, ni muhimu sana kueneza elimu ya nini albinisim, kwa sababu elimu hii kama haijafika katika jamii ndio kunapelekea kuwa na ufahamu mbaya kuhusu watu hawa” amesema naibu spika.

Katika hatua nyengine Mgeni ametoa wito kwa waajiri nchini kuajiri watu wenye ulemavu, amesema ipo sera hiyo ili kila mmoja afaidi fursa za ajira kwa lengo la kuwanusuru kuingia mitaani na kuomba.

Akizungumza kabla ya mgeni rasmi mkuu wa mkoa wa Mjini Maghrib Ayoub M Mahmoud ameitaka taasisi ya All Albinism ambayo imeanzishwa rasmi nchini kwa shabaha ya kutatua changamoto za watu wenye ualbino  kuwafikia watu hao ili kujua kiundani changamoto mbalimbali zinazowakabili na kuona kuona namna bora ya  za kutatua changamoto hizo.

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib amesema, aliyeandaa kampeni ya kuwafikia watu wenye ualbino anapaswa kuungwa mkono hivyo yupo tayari kuunga mkono juhudi hizo kwani hao ni watu wa kawaida na yoyote anaweza kuzaa mtoto wa aina hiyo.

“tukuahidi kuwa tutakuunga mkono, uweze kuwafikiwa wazazi na walezi wa watoto wenye ualbino, kwani ni wahusika wakuu wa watoto hawa” amesema Ayoub

Awali kiongozi wa taasisi ya All Albinism ndugu Yumna Mmanga amesema kuwa ualbino sio jambo la kushitusha kwani ili mtoto azaliwe na ualbino ni lazima arithi kwa mama na baba na sio kosa la mama pekee.

“ukijiona wewe huna ualbino ujue una vinasaba vya ualbino ukiona au kuolewa na mtu mwenye vinasaba vya ualbino unaweza kuzaa mtoto mwenye ualbino” amesema Yumna ambae pia anaishi na ualbinism ameelezea namna gan albino anatakiwa aishi na kuiomba serikali na wahisan kuwapa kipaombele watu wenye ualbinism ktk fursa za ajira.