ACT Wazalendo wanena, tuhuma za upachuaji Bendera za chama chao.

Imeandikwa na Mwandishi wetu – Zanzibar.

Mshauri mkuu wa chama cha ACT Wazalendo Maalim Seif Sharif Hamad amesema chama hicho kinataarifa za uhakika za kutaka kufanyika njama za uhalifu katika ofisi za chama cha ACT Wazalendo Unguja na Pemba kwa lengo la kutaka kuwakamata viongozi wake.

Amesema njama hizo zimepangwa kuanza kutekelezwa kuanzia jana na sehemu ya malengo ya mpango huo ni kutaka kukamatwa kwa Viongozi wa chama hicho ili kukivuruga na wafanikishe malengo yao.

Maalim Seif ameyaeleza hayo leo huko katika ofisi za ACT Wazalendo Vuga mjini Unguja alipokua akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali.

Maalim Seif alisema, jana kulianza kufanyika zoezi hilo kwa kutaka kupachua bendera za chama katika ofisi zao lakini wananchi wa Pemba walikua tayari kwa lolote hatimae vijana hao walishindwa kutekeleza maazimio yao hayo.

“kumeratibiwa kufanyika njama hizo wakiamini kufanyika kwa matukio hayo kutasababisha hasira kwa viongozi wa chama hicho ili kuwakamata” alisema Maalim Seif.

Aidha ametoa wito kwa viongozi wa chama hicho pamoja na wapenda amani wote walinde ofisi zao na wasiruhusu kwa yoyote kutaka kuingia na kuharibu afisi hizo.