AFCON 2019: Mambo matatu yaliyoifanya Kenya kuichapa Taifa stars

 

Mechi ya jana ya kombe la taifa bingwa Afrika kati ya Kenya na Tanzania ilisubiriwa kwa shauku kubwa wapenzi soka kote barani.

Lakini katika kanda ya Afrika Mashariki,mechi hiyo ilikuwa na uzito zaidi kwasababu haikuwa mechi ya kawaida

Ilikuwa mechi ya kuamua heshIma na taadhima na kuweka mambo sawa katika ya mashemeji wawili.

 

Ilikuwa na uzito wa bendera ya taifa na utaifa na baada ya dakika tisini mbabe kati yao angejulikana.

Ni kutokana na hizo sababu ndio kama ulikuwa makini mitandao ya kijamii ilifurika picha, video na ujumbe wa kila aina.

SamattaHaki miliki ya pichaCAF
Image captionSamatta amefunga bao lake la kwanza kwenye michuano ya AFCON 2019

Swali likiwa moja tu ,Ni nani atakuwa juu?

Wanaomfahamu Pierre Liquidi wanaafiki anavyopenda kusema maneno hayo.

Basi ngoma ilikaanza na ikawa ni kama kupimana nguvu na vijana wa Taifa Stars na Harambee Stars wakijaribu wote kuiweka timu zao mbele.

Mbwana Samatta akiwa eneo la hatari piga shoti mlinda lango Patrick Matasi akapangua ila Simon Musuve akamalizia kazi.

Kenya ikasalia kimya kwa muda na kabla ya muda wa mapumziko,Michael Olunga ama Engineer wanavyomuita mashabiki wa Kenya akapiga bao la kufa mtu na kurejesha matumaini lakini hata kabla wamalize kusherehekea Samattaaaaaaaa!!! akacheka na nyavu kwa mara ya pili na kuwaweka Wanzania mbele ya Wakenya.

Kipindi cha pili Johanna Omollo na Olunga wakafanya kilichowapeleka Misiri na kuizamisha Taifa stars.

Michael Olunga celebratesHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMichael Olunga (kushoto) amekuwa mwiba mkali kwa safu ya ulinzi ya Tanzania

Kwa mechi hiyo mashabiki wengi hawakuamini kilichotokea.Licha ya mchezo wa kufurahisha na kusisimua na Taifa Sars kuongoza katika kipindi cha kwanza na baada ya dakika tisini,wakaachwa hoi bila pointi tatu walizopigania.

Ilikuaje Kenya ikaipiku Tanzania?

1. Mikakati

Makocha wa Kenya kwa muda wamekuwa wakilaumiwa kwa kutokuwa na mikakati ya kutosha wanapounga kikosi pamoja na kufanya mabadiliko mabovu wakati mechi inapoendelea.

Kuanzia Reinhard Fabisch, Jacob ‘Ghost’ Mulee na hata kocha wa sasa mfaransa Sébastien Migné.

Kabla ya kikosi cha Kenya kuelekea Misri, Migné alilaumiwa kwa kuwaacha wachezaji wenye uzoefu kama mshambuliaji matata Allan Wanga na badala yake kumbeba Paul Were licha ya kuwa alikuwa anauguza jeraha.

Kufuatia kupoteza mechi 2-0 dhidi ya Algeria,kocha Migne aliwachezesha Johanna Omollo, David Owino and Eric Ouma na kuwapumzisha Eric Johanna, Philemon Otieno and Dennis Odhiambo.

Katika mechi dhidi ya Taifa Stars,baada ya Tanzania kufunga,alimwondoa mchezaji wa safu ya kati Francis Kahata na kumuingiza John Avire aliyesababaisha foul iliyopeleka Kenya kupata bao la kwanza kando na kunoa makali ya safu ya ushambulizi.

Hii ilibadilisha mizani na kuifanya Tanzania kuwa na wakati mgumu kuudhibiti mpira haswa katikati mwa uwanja ili kufanya mashambulizi.

2Uwekezaji kwenye timu

Serikali ya Kenya imekuwa ikilaumiwa na mashabiki wa soka nchini kwa kutowekeza katika vya kutosha katika timu ya taifa.

Wakati wa kufuzu kwa kipute hiki,serikali ilidai haina fedha za kutosha kuwalipa marupurupu wachezaji waliokuwa wakielekea kupambana na Ethiopia.

Hata hivyo serikali ilibadili mkondo mara timu ilipofuzu.

Rais wa shirikisho la kandanda nchini Kenya (FKF) Nick Mwenda alidai kuwa wachezaji wote kwenye kikosi wangepokea anagalau dola 7,500 kila mmoja kama marururupu.

Pamoja na hayo,aliongezea kuwa kila mchezaji angepokea dola 2,500 kwa kila mechi watakayoshinda.

Haya kwa sasa fanya hesabu tu!

Kwa jumla serikali ilikuwa imetenga dola milioni 2.1 kuisadia timu ya Harambee Stars kujitayarisha katika michuano ya Afcon.

Pesa hizo zilitumika kukituma kikosi hicho Ufarasa walikomenyana na Madagascar na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Bilashaka matayarisho hayo yaliyowezeshwa na fedha kuliwapa vijana wa Stars motisha zaidi.

3.Historia

Historia huwa sehemu kubwa sana ya soka.Kila mara mashabiki hukumbushana na kijitanua vifua kwa mahasidi wakimbushana ushindi wa jadi.

Mashabiki huenda wakasahau kumlipa mtu deni ama hata kuoga lakini si siku timu yao iliposhinda kombe fulani ama kumshinda hasimu wao mkubwa.

Na hapa pia historia ilirudiliwa.Harambee Stars na Taifa Stars zilikuwa zimekutana mara 48 kabla ya mechi ya jana.

Na kwa mechi hiyo,Kenya ilikuwa imevuna ushindi zaidi.Kwa mechi hizo 48,Kenya ilikuwa imeishjinda Tanzania mara 23(47.9%),kutoka sare mechi 10 (20.8%) na kupoteza mechi 15 (31.3%).

Timu hizi mbiliz zilikutana mwanzo mwaka 25 Septemba 1971 na mechi hiyo ikaishia sare ya 1-1.

Hata hivyo timu hizi mbali haziachani mbali katika msimamo wa FIFA kwani Tanzania ilikuwa nafasi ya 134 na na kenya 130 kkabla ya mechi ya jana.Kwa wengi wa mashabik nchini Kenya,watasema,ukivuliwa chutama. Raundi hii walimvua Taifa Stars.

Kwenda Mbele itakuaje?

Ushindani kati ya Tanzania na Kenya utazidi kuwepo.Wanavyitana wenyewe kama ‘mashemeji’ ina maana wana uhusiano amabao hauvunjiki hivi karibuni.

Kweli Diamond Platinumz,Ali Kiba wamepata wachumba Kenya.

Wakenya na vilevile wana ya kwao.Wanacheza Tetema na Chekecha.Lakini jana ilikuwa kukanyagana na kwenye shemeji alikanyagwa.

Mechi ya makundi ya kombe la Afcon itaendelea.Kenya watapambana na Senegal,wote wakiwa na pointi tatu inagawaje Kenya ina uzuri wa mabao.

Tanzania watakutana na Algeria,ambao ndio viongozi wa kundi C kujaribu kuvuna pointi tatu.

Watashikilia imani kuwa Watamshinda kwa mabao mengi wakiamini Senegal atamchapa Kenya ili warudi wote Afrika Mashariki. (bbc)