Ajira za Watoto bado ni tatizo linalo katisha haki zao.

Ajira za watoto bado ni tatizo linalopelekea  baadhi ya  watoto kukosa haki  ya elimu  katika baadhi ya maeneo ya kisiwa cha Pemba hasa katika maeneo ya visiwa vidogovidogo vilivyozungukwa na bahari.

Kisiwani Fundo, watoto wameshuhudiwa wakiwa katika harakati za kujipatia pesa il- hali wakati huo wanapaswa kuwa skuli au Madrasa kuendelea na masomo, ukizingatia pia kufanya kazi ngumu kwa watoto ni hatari kwa afya zao.

Pemba Today kupitia mwanahabari wake Amina Ahmed aliyepo katika ziara maaluma ya utafutaji wa habari na matukio kisiwani humo, ameshuhudia hilo wakati wa  asubuhi,  anasema, baadhi ya watoto  wanaonekana wapo  katika harakati za kuendesha Mitumbwi kuwavusha watu wanaoingia na kutoka kisiwani humo.

Nahoza/Dereva wa chombo hiki ni mtoto ambae anastahiki muda huu kuwa skuli au Madrasa.

Kazi yote hiyo huifnaya muda wa masomo wakati wenzao wakiendelea  kupata haki hiyo madarasani.

Kazi hizi kufanywa na watoto kisiwani humo si jambo la kushangaza na  imeshazoeleka kwani hata watoto wakike nao pia hushiriki kufanya hivyo.

Chombo cha Pili, ni watoto wanaoondoka na chombo hicho kuelekea maji makubwa kwa shuhuli za uvuvi.

Anasema Amina “nilizungumza na baadhi ya watoto hao, walinijibu kuwa, wanafanya kazi na kama hakuna kazi ndio wanakwenda skuli na chuoni”

Ipo haja kwa serikali kupitia  wizara ya Elimu na wadau  wengine kulitazama jambo hili kwa jicho la huruma ili kuepusha wimbi kubwa la watoto kukosa elimu pamoja na kuandaa mikakati madhubuti itakayokomesha vitendo hivyo.

Camera ya Pemba Today pia imemnasa mtoto akionekana kuwa katika harakati za kukileta chombo ufukweni ili kuendelea na usafirishaji wa abiria wanaotaka kuingia na kutoka kisiwani humo.

Kwa uchache, zaidi  ya watoto kumi wameonekana katika Mitumbwi tofauti  wakiendeshana   kuelekea  maji makubwa  kufanya kazi ya uvuvi  wa samaki ,  wengine wakiogelea na wengine wakisafirisha watu.