Amina, mwanasiasa chipkizi anaekuja kwa kasi, alisaka jimbo la Mtambile kwa ADA-TADEA

 

 

IMEANDIKWA NA HAJI NASSOR, PEMBA

……mwaka huu ndio anatimiza miaka 25 tokea aanza kung’ariwa na hali ya hewa ya dunia.……

Ni mwemba mba, mwekundu wa wastani, ni mcheshi wa kupindukia na hapendi kuuvaa ugeni kwenye makundi ya watu.

Paji lake la uso linakwenda sambamba na haiba ya moyoni mwake, na mazungumzo yake ya kwaida, hupenda kuingiza lugha ya kigeni ijapokuwa neno moja.

“Karibu nyumbani, na mujiskie ‘free’ yaani huru,’’ ndio maneno ya mwanzo nilipobisha hidi kwao mgombea huyo wa ubunge wa Jimbo la Mtambile kwa tiketi ya chama cha ADA-TADAE Amina Muhammed Ali.

Amina kwa sasa anaishi Mkoani kijiji cha Mfenesi mazizi, yaani ndani ya mji wa Mkoani, ingawa kwa sheria za tume anahaki ya kugombea jimbo la Mtambile kwa vile hapo ni kwao pia.

Nikiwa nimekaa nae eneo la kupokelea wageni ndani ya nyumba yao, huku akiwa na kanga yenye nembo ya chama chake, alipangua kila sualia amabalo nilimuuliza.

AMINA NA SIASA

Alianza kuipenda siasa tokea akiwa skuli ya sekondari kidato cha nne ya ‘Green Acers’ ya sekondari jijini Dar-es Salaam, ambapo anasema lakini haikumvurugia masoma yake, kwani alikua anatenga muda.

Kwa mwaka huo wa 2014 hadi 2015, anasema akivutiwa mno na Makamu wa rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania mama Sami Suluhu Hassan.

Kwake anasema kama kuna mtu ambae alimshawishi kwa kazi zake na leo mwaka 2020 akijikuta anagombea ubunge Jimbo la Mtambile wilaya ya Mkoani basi ni Samia Suluhu Hassan,

Alikuwa nanafuatilia mno tv, na hasa vipindi maalum au taarifa ya habari kumuangali namna Samia anavyozungumza na wakati mwengine apotoa hutuba zake.

“Mimi Samia ndie mtu kwangu ndio mfano na kigezo cha kuingia kwenye siasa na kutafuta uongozi kupitia Jimbo la Mtambile,’’anasema.

Amina anasema kumbe hakuna mwanamke asiyeweza uongozi, maana Samia ameshika nafasi kubwa ambayo tokea mwaka 1964, akiwa mwanamke wa kwanza.

Samia kwangu ndio kigezo, na sasa naanza kuvinyemelea na kuvivaa viatu vyake kisiasa na uongozi, akisema ana hakika hashindwi na kitu.

“Heshima, nidhamu, kujiamini, kukubali kuelekezwa na uwajibikaji ndio mambo ambayo anayo Samia na mimi sasa naanza mdogo mdogo hadi kileleni,’’anasema.

Nilimuuliza kwanini asiingie ndani ya CCM ambayo aliko Samia, akajibu kuwa nchi imeridhia vyama vingi makusdi, ili kila mmoja akimbilea apendako.

“Ni kweli ‘role mode’ wangu yeye yuko CCM na mimi nimeanza na chama cha ADA-TADEA lakini hii ndio demkrasia, cha msingi ni kuzingatia misingi ya uwajibikaji hata ukiwa chama chengine,’’anasema.

Mwanzoni mwa mwaka huu 2020, mgombea huyo wa ubunge wa Jimbo la Mtambile alimaliza masomo yake ya diploma ya uhasibu katika chuo cha ‘Tanzania Institute Accountancy jijini Dar- es Salaam.

KILICHOMVUTA KUOMBA NAFASI HIYO

Amina Muhammed Ali, mgombea huyo wa Ubunge wa Jimbo la Mtambile kwa tiketi ya ADA-TADEA anasema anamambo lukuki yaliompelekea kuomba nafasi hiyo.

Kipaumbel chake anasema ni kuona anaimarisha suala la elimu kwa skuli zote za sekondari na hasa eneo la sayansi, ili kuona skuli za jimbo hilo zinaingia kwenye skuli 10 kwa Tanzania.

Anaumwa mno, kuona kila mwaka skuli za Zanzibar zikiwemo za Jimbo la Mtambile zinaburura mkia, na kujikusanyia matokea mabaya.

Mwarubaini wa hilo, anasema anao yeye kama akipewa ridhaa na wapiga kura wa Jimbo hilo, ikiwa ni pamoja na kutafuta waalimu au vijana wenye ufahamu wa masomo ya sayansi na kuwakabidhi kwa skuli hizo.

“Bado masomo ya sayansi hakujawekwa mkazo wa kutosha, na ndio maana skuli zetu za jimbo la Mtambile hazijawahi kuingia kwenye kumi bora kitaifa, lakini hilo jepesi nikipata riadhaa,’’asimulia.

Anaona waalimu hata hao wachache waliopo hawajahamasishwa kutokana kazi yao ngumu wanayoifanya, hivyo kwa baadhi ya wakati hupoteza mwelekeo.

Akikabidhiwa Jimbo hilo kwa miaka mitano ijayo, mgombea huyo kupitia ADA-TADEA anakusudia kuvimulika vikundi vya ushirika vya akina mama, ili sasa view kimbilio.

Anasema vipo kadhaa lakini vimekumbwa na changamoto kama vile usajili na ukosefu wa elimu ya kuviendesha vikundi hivyo.

Anawaahidi wananchi wa Jimbo la Mtambile, kuwa akipata ridhaa atawapatia mitaji na mtaalamu wa matumizi ya fedha hizo ili vikundi vyao view mfano na majimbo mengine.

“Kila mmoja ni shahidi kuwa, ajira za serikali hazitoshi, sasa kama kuna vijana au wanawake wamejiekeza kwenye sekta binafsi lazima tuwaneemeshe,’’anasema.

Anasema hata makundi ya watu wenye ulemavu wa aina mbali mbali, nao wana haki ya kutengenezewa mazingira ya kuweza kujiajiri kwa kuanzishiwa mfuko wao maalum.

“Kama kundi la watu wenye ulemavu tunawahitaji kwenye kupiga kura, basi hata baada ya kupata nafasi hizo nao tuwakumbuke kwa namna yake, na hili naahidi nitalifanya,’’anasema.

Michezo anasema ni sehemu kubwa ya kuzaa ajira, hivyo anakusudia kuwa na mashindani maalum ya kuvuna vipaji, kupitia michezo tofauti.

Amina Muhammed Ali, anaetimiza miaka 25 ya kuzaliwa, anasema waalimu wa madrassa kama akiwa mbunge wa Jimbo la Mtambile atawapatia posho maalum, ili kazi yao waifanye kwa ufanisi.

“Inawezekana wapo waalimu wamekuwa wahawana nafasi nzuri ya kusomesha, kutokana na kukosa fedha za kujikimu, sasa kama nikichaguliwa hilo litalifanya,’’anasema.

Ili kutimiza azma na utekelezaji wa ahadi hizo, Mgombea Amina anawanasihi wapiga wa Jimbo la Mtambile wasizipoteze kura zao na wamtilie yeye wakati ukifika.

“Dhahabu inayokuja kuling’arisha Jimbo la Mtambile ni chama cha ADA-TADEA kupitia mimi kijana Amina Muhammed Ali, ila kura zao wakizipoteza wanaweza kujuta,’’anasema.

AINA YA KAMPENI ZAKE

Anasema hakuingia kuomba nafasi hiyo akitegemea ruzuku kutoka chamani mwake, bali ameshajipima na kuona anaweza kulimaliza jimbo lote kwa rasilimali yake.

“Hata boda boda na ngalawa nitatumia au gari ya abira nitatumua ili kuhakikisha shehia zote zilizomo ndani ya jimbo la Mtambile nimekutana na kuwaomba kura wananchi,’’anasema.

Anasema kampeni sio lazima kufanya mkutano wa hadhara kama vinavyofanya vyama vingine, bali cha msingi ni kukutana na wapigakura kwa njia yoyote ile.

“Mimi hata kwa njia simu, ana kwa ana, kwenda kwenye mikuanyiko kama vile masokoni, kwenye vikundi vya wanawake kama hisa mute nitakwenda na kuomba kura,’’anafafanua.

Yeye kubwa analoomba ni vyombo vya habari kumuandikia habari zake, kwani hata kama hana mafuta ya kuwapa waone kuwa kila mgombea anahaki ya kuvitumia vyombo vya habari.

WANANCHI WA MTAMBILE

Hafidh Muhidini Kassim wa Kisiwa panza, anasema wameshakuwa na wabunge kwa vipindi vitano lakini hawajaona matunda kwa wao walioko visiwani.

‘Kwa mwaka kwa vile tunamgombea uwakilishi na huyu mbunge nae ni mwanamke, lazima tuhamasishane kuna wanasimama,’’asema.

Mwajuma Bakari Nassa wa Kangani anasema tayari wameshakutana na mgombea huyo ubunge, na wamevutiwa mnona na ahadi ya kuviirisha vikundi vya ushirika.

Amina Hemed Mbarawa na Asha Muhusin Omar wote wa Kisiwa panza, wanasema kazi zao ya kilimo cha mwani huwenda kikapata mkombozi mwaka huu.

“Kama atatuletea mataalamu na mashine ya kuusarifu mwani, ni jambo jema maana kazi ya kilimo cha mwani ni kubwa lakini kipato ni kidogo mno,’’anasema Amina.

Faida Said Bakari anasema lazima kura zao kwa mwaka huu wamunge mkono mgombea huyo, maana jimbo lao lilikaliwa kwa muda mrefu na viongozi wanaume.

“Kiongozi mwanamke ndie anaejua shida zetu sisi wanawake wenzake, hivyo niwaombe wapigakura na hasa wanawake kwa mwaka huu tisifanye kosa,”anakumbusha Faida.

Jimbo hilo la Mtambile lililopo wilaya ya Mkoani mkoa wa kusini Pemba, pamoja na mgombea huyo wa ubunge wa tiketi ya ADA-TADEA lakini hata Asha Said Suleimana anagombea uwakilishi kwa tiketi ya CUF.

MWISHO