Baba adaiwa kumbaka mtoto wake wa kumzaa Pemba

Imeandikwa na Salmin Juma – Pemba

Email:salminjsalmin@gmail.com

‘’sisi kama TAMWA tunaudhika sana kusikia matukio haya kila siku lakini nikwambie, kwa hili  tutasimama kidete kuhakikisha  baba huyu anachukuliwa hatua za kisheria ikibainika ni mkosa,  ili haki itendeke tunaumia sana”

Hiyo ni kauli ya bi Fat-hiya   Mussa Said mratibu wa Chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania Upande wa Zanzibar, ofisi ya Pemba, alipokua akizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa tukio la baba kudaiwa kumbaka mwanawe wa kumzaa huko Taifu kakazini Pemba.

Akizugumza mbele ya Mwandishi wa habari hizi Bi Fat-hiya alisema, kadiri ya siku zinavyosonga ndivyo inavyonekana matukio hayo kuzidi, lakini TAMWA kwakua ni wadau wa kupinga mambo hayo wamejikubalisha na hawatorudi nyumba, wataendelea na mapambano hadi kuona jamii hasa ya wanawake na watoto inakua sawa.

“uwepo wa taarifa za tukio hili umetuumiza sana,, lakini tutalisimamia hadi mwisho wake, kwa sababu mambo mengine ni aibu kubwa, baba kumbaka mwanawe ni hatari” alisema Mratib huyo.

Kwa uapande wake Kamanda wa Polisi mkoa wa Kaskazini Pemba Shehan M Shehan amekiri kutokea tuhuma hizo za baba kudaiwa kumaka mtoto wake wa kumzaa.

Alisema, tukio hilo limetokea Taifu Wete siku ya tarehe 30/11/2019 majira ya saa 3 usiku  ambapo mtuhumiwa (jina linahifadhiwa ana miaka 43) ambae ni baba wa mtoto anaedaiwa kumbaka.

“alimuingilia mtoto wake wa kumzaa, ana miaka 12, alikua analelewa na Shangazi yake huko Wingwi, tarehe hiyo ndio siku aliyomuingilia” alisema kamanda huyo.

Akiendelea kujibu maswali ya mwandishi wa habari aliyetaka ufafanuzi zaidi wa tukio hilo kamanda alisema, mtuhimiwa aliachana na mkewe, na mtoto huyo alikua akilelewa na shangazi yake Wingwi Njuguni, lakini baada ya muda, baba alikwenda kumchukua mwanawe na kuishi nae nyumbani wakiwa peke yao.

“alikua analalanae katika godoro moja” alisema Kamanda.

Kwa mujibu wa kamanda Shehan, siri ya tukio hilo ilibainika baada ya wananchi kumtilia shaka mtuhumiwa kwa mwendendo wa maisha yake na mwanawe na ndipo walipoamua kupeleka taarifa kwa Sheha wa shehia hiyo na  kisha kufika polisi na baada ya uchunguzi ndipo kulipobainika tukio hilo.

Alisema, mtuhimiwa yupo chini ya mikono yao na taratibu zitakapomalizika watamfikisha mahakamani kujibu tuhuma hizo ili kuruhusu sheria kuchukua mkondo wake.

Katika hatua nyengine kamanda Shehan alisema Jeshi la Polisi mkoa huo linaendelea kumshikilia Kijana Suleiman Zahor Omar (28) wa Bopwe Wete kwa kosa la utoroshaji.

Alisema tukio hilo limetokea siku ya tarehe 04/12/2019  “majira ya saa moja usiku,inadaiwa alimtorosha mtoto huyo mwenye miaka 17 kutoka Gando hadi Mangwena, tulipomfuatilia tulimkuta na mtoto huyo ambae aliaga kwao anakwenda kununua chipsi na hakurejea tena”alisema kamanda Shehan.

Kamanda alitoa wito kwa wananchi, kuacha vitendo vya udhalilishaji kwani Jeshi la polisi mko huo limejipanga vyakutosha kuwashuhulikia wote watakaotuhumiwa na makosa hayo.