CCM : hawatomuonea mtu katika kutenda haki

Katibu wa CCM mkoa ambae pia ni mwenyekiti wa sekretarieti ya mkoa mjini kichama.

Chama cha mapinduzi CCM mkoa wa mjini kimesema kuwa hakitomuonea mtu yoyote ambaye anasifa za kugombania nafasi mbali mbali ikiwemo ubunge, uwakilishi , diwani kutokana na katiba ya chama hicho inavyoeleza .

Akizungumza kwa nyakati tofauti na kamati za siasa ,kamati tekelezaji ya jimbo na mabalozi katika jimbo la mpendae bondeni na jimbo la amani kwa wazee katibu wa CCM mkoa wa mjini kichama ambae pia ni mwenyekiti wa sekretarieti ya mkoa ndg, Abdallah Mwinyi Hassan amesema kila mwanachama anahaki ya kuchagua na kuchaguliwa .

Amesema chama cha mapinduzi kina kinamuheshimu kila mwanachama anajihisi anasifa za kugombania na ndio maana katiba ya chama hicho ikaweka wazi kila sifa kwa kugombania nafasi ndani ya chama.

Aidha amesema kuwa ni marufuku kwa wagombea kupita majimboni na kuanza kupiga kampeni kabla ya wakati wake kufika na badala yake wafuate maelekezo yanayotolewa na chama hicho .

” ni marufuku kwenda katika majimbo kuanza kujinadi kwani wakati wake bado haujafika.”” amesema nd, abdallah.

Sambamba na hayo amewataka kutokubali kutumiwa na wasio penda maendeleo ya nchi na badala yake wawe makini katika kuchagua viongozi wazalendo .

Mapema katibu wa siasa na uenezi mkoa wa mjini kichama ndg, Maulid Mussa khamis amesema chama cha mapinduzi kinahitaji kushinda katika chaguzi zote za dola hivyo ni vyema kushirikiana kwa pamoja ili kukipa ushindi katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika oktoba mwaka huu.

Nao wanachama wa chama cha mapinduzi ccm wamesema watahakikisha wanachagua viongozi walio kuwa imara na wenye sifa zote ili waweze kuwatumikia na kuwaletea maendeleo ndani ya majimbo yao.