CHADEMA waanika sababu za kujitoa uchaguzi serikali za mitaa

 

Chama cha demokrasia na Maendeleo Chadema cha nchini Tanzania, kimejitoa katika mchakato wa uchaguzi wa serikali za mitaa unaondelea nchini humo.

Mwenyekiti wa chama hiko cha upinzani ametangaza kutoshiriki katika uchaguzi unaotarajiwa kufanywa baadae mwezi huu kwa madai kuwa kufanya hivyo ni kuendeleza uonevu unaofanywa katika mchakato wa uchaguzi huo.

Uchaguzi huu unatarajiwa kufanyika novemba 24, ni uchaguzi unaongozwa kwa kanuni za uchaguzi wa viongozi wa mamlaka za Serikali za Mitaa ngazi ya Vijiji, Vitongoji na Mitaa katika mamlaka za Wilaya na mamlaka za Miji nchini Tanzania.

”Katika misingi hii ndugu watanzania, tumelazimika kukaa na kutafakari, baada ya vikao tulivyofanya kwa siku nzima ya leo, tumeamua kutobariki uchaguzi huu, ubatili umefanywa na serikali, na chama cha mapinduzi, sisi kama chama hatutashiriki katika uchaguzi huu, hatuko tayari kujihusisha na ubatili, anasema Mbowe mwenyekiti wa chadema mara baada ya mkutano wao wa kamati kuu.

”Tunawajua viongozi wengi wa chama cha mapinduzi ambao hata kusoma wala kuandika hawajui, jiji la Dar es salaam pekee tulikua na mitaa zaidi ya 500, lakini wamekatwa na kubaki mitaa 24, hali ni hiyo hiyo katika mitaa ya miji mingine, tunaomba rais asikie, hili ni taifa ni mali ya watanzania sio chama tawala” anaongeza Mbowe.

mbowe
Image captionFreeman Mbowe kiongozi wa chama cha upinzani Chadema

Wafuasi wa chama hicho wameonesha kufarahishwa na hatua hiyo kutokana na madai ya kukatwa katika maeneo mengi ya nchi.

”Mimi nilitegemea kamati kuu itoe maamuzi haya, na ni maamuzi ya busara, mfano kwa Dar es salaam tumekua tumejiandaa kweli kweli mbali na kuzuiwa, hebu fikiri zaidi ya mitaa 130, tumeweka wagombea lakini wote wameondolewa wamebaki 15 tuu , na hao bado wana vikwazo, unaendelaje na uchaguzi unaachiwa mitaa mitatu tuu?” anasema Makongoro Mahanga mmoja wa kiongozi wa chadema.

Zoezi linaoendelea hivi sasa ni uteuzi mara baada ya kurudishwa kwa fomu za wagombea wa vyama mbalimbali, lakini kwa upande wa Chadema na vyama vingine vya upinzani wagombea wake wamekua wakienguliwa kwa madai kuwa hawajakidhi sifa katika kujaza fomu zao.

Kwa mujibu wa chama cha Chadema, katika mkoa wa mwanza pekee wagombea wa chama hiko zaidi ya Elfu moja wameondolewa sifa za ushiriki katika uchaguzi huo.

Kwa upande wa chama kingine cha upinzani cha ACT wazalendo wanasema kuwa wagombea wake zaidi ya 200 wameondolewa bila sababu, na baadhi wakiambiwa chama chao hakipo katika orodha ya msajili wa vyama vya siasa.

chadema
Image captionBaadhi ya viongozi wa chadema

”Wagombea wetu jumlya ya 200 mpaka sasa takwimu zetu wamenguliwa bila kupewa sababy, hivyo tumeitisha kamati ya dharura ya chama ili kutafakari hali hii mbaya ya kisiasa” anasema kaimu katibu mkuu wa ACT Doroth Semu.

Wizara inasema nini hasa juu ya za tuhuma za upinzani?

Kumekua na tuhuma mbalimbali hasa kutoka upinzani nchini Tanzania juu ya dhulma ya uchaguzi huu, wapinzani wanadai kuwa wamekua wakiondolewa bila sababu za msingi, lakini pia wakuu wa wilaya wakitumika vibaya kuwapa vitisho wagombea wa upinzani.

Kutokana na hatua hii ya Chadema kujitoa, Waziri wa nchi ofisi ya rais tawala za mikoa na serikali za mitaa Suileman Jaffo anasema kuwa uchaguzi upo pale pale, tarehe 24 ya mwezi huu kama ilivyokua imepangwa hapo awali.

Waziri Jaffo anasema kuwa atahakikisha ofisi yake itahakikisha haki itapatikana kwa madai yoyote ya dhulma.

”Ofisi yangu inachukua hatua na kuhakikisha tutachukua hatua, nilipata kesi maeneo ya mkoa wa songwe na baadhi ya maeneo ya Dar es saalam, na nikatoa amri fomu zipokelewe na kama litatokea tatizo lolote tutashughulikia.

kwa upande wa chama tawala hali ikoje?

Mapema hii leo, katibu na wa itikadi na uenezi wa CCM, chama tawala nchini humo, aliitisha mkutano na waandishi wa habari, na kueleza hali ilivyo kwa chama chake lakini pia kuwajibu baadhi vya vyama upinzani kwanini wamekua wakiengulia katika mchakato wa uchaguzi wa serikali za mitaa.

”Wenzetu hawa wamekua wakikosea sana katika kujaza fomu, ukiwa na haraka mfano mtaa unaitwa Sinza A, lakini wewe kwa kuvurugwa kwako unaandika Sinzaa basi hapo lazima uondolewe, wagombea wengi hawa ni watu ambao hata kazi hawana, hawajui kusoma wala kuandika, unategema nini hapo?” anasema Humphery pole pole katibu wa uenezi wa CCM.