Dk. Mwinyi akiwa Pemba asema, ushindi wa CCM hautaki tochi

 

IMEANDIKWA HAJI NASSOR NA THUREA GHALIB, PEMBA

 MGOMBEA urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi ‘CCM’ Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema katika kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 28 mwaka huu, chama hicho kina kila sababu ya kupata ushindi mnono, kutoka na kufanya kamapeni za kistaarabu na kisayanasi kwa wananchi wote.

Aliyasema hayo wakati alipokuwa akizungumza na  wajumbe wa kamati za siasa, makada wa chama cha Mapinduzi, Mabalozi wa wenyekiti wa mashina, ukumbi wa skuli ya sekondari ya Fidel Castro Wilaya ya Chake Chake, Mkoa wa kusini Pemba.

Alisema kwa kushirikiana na wenzake wamekuwa wakijitahidi kuhakikisha kampeni za chama hicho zinakuwa bora na imara kwa kule kuyafikia makundi yote ya wananchi wa Zanzibar.

Alisema, hilo na mengine ndio ambayo yatakihakikisha chama cha Mapinduzi kinaibuna na ushindi usio na malalamiko, kwenye uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.

Alieleza kuwa, wamekuwa wakikutana na  makundi kama ya wafugaji, wavuvi, wajasiriamali, mama lishe, wafanya wa taasisi za umma jambo ambalo limewavutai mno wananchi hao.

“CCM kuelekea uchaguzi mkuu mwishoni mwa mwezi huu, ushindi unakuja na hauna wasi wasi, maana tumekuwa tukifanya kampeni za kisayansi na kiungwana ambazo hazina viashiria vya uvunjifu wa amani,’’alisema.

Katika hatua nyingine Mgombea huyo wa urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Dk. Hussein Ali Mwinyi, alisema kila mwanachama wa chama hicho, lazima ahakikishe ifikapo Oktoba 28, anajitokeze kukipigia kura chama chake.

Alisema haya wale wa vyama vyengine iwe ni ACT-Wazalendo, CHADEMA, CUF, AAFP, NRA, ADC, UPDP ni vyema wakawapigia kura wagombe wote wa CCM ili chama cha mapinduzi kuleta mandeleo.

“Mabalozi wote wa chama chetu, wakifanyan jukuumu lao vizuri na wakatoa watu wao wote kujitokeza kukipigia kura chama cha Mapinduzi, basi hakuna wasiwasi wa kupata ushindi mkubwa kuliko tunaotarajia kuupata,’’alisema Dk. Mwinyi.

Mgombea huyo alitakata Viongozi wa Chama Kuhakikisha kuwa waWAnandaa Mabalozi kufanya majukumu yao, endapo kutakua na changamoto zozote basi wasisite kuzielezea ili wapate kusaidiwa.

Akizungumzia kuhusu suala la kuleta maendeleo Dk. Hussein alisema kuwa amezamiria kufanya mapinduzi makubwa ya uchumi hapa Zanzibar, ili kuwaletea maendeleo wananchi wote.

“Nikizungumzia uchumi namanisha sana uchumi wa bluu, ndani yake muna uvuvi wa kisasa, uchimabaji wa mafuta na gesi na kuna viwanda, tukifanya haya mambo makubwa manne uchumi wa nchi yetu itabadilika,”alisema.

Akizungumzia sula la amani Dk. Hussein aliwasihi wananchi kutunza na kuendelea amani waliyonayo, na wasikubali kurubuniwa na baadhi ya watu wasioiakia mema nchi.

Alisema kuna baadhi ya viongozi wanatabia ya kuhamisha uvunjifu wa amani, hivyo wasiwasikilize na badala yake waendelee kuitunza tunu hiyo.

Aidha aliwatoa hofu wanachama kuwa ifikapo tarehe 28 Oktoba mwaka huu, wananchi wote watapiga kura kwa hali ya ulinzi na usalama, kwani Serikali imeshajipanga kuhakikisha hakuna atakaezuiwa na vikundi vya watu.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Abdalla Juma Sadala ‘Mabodi’ amesema kuwa mabalozi wa chama cha CCM ndio jeshi kubwa, ambalo limekuwa likijitolea katika kuhakikisha linapigania ushindi wa chama hicho.

Alieleza kuwa, mabalozi wanakila sababu ya kupongezwa kwa kazi nzuri walizokuwa wanazifanya, kuanzia kipindi cha ugwawaji wa vitambulisho hadi kufikia sasa, katika kukitafutia ushindi chama cha Mapinduzi.

Nae Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa kusini Pemba Yussuf Ali Juma, alisema kwa niaba ya mabalozi wote watahakikisha wanasimamia na kuhakikisha wanakipatia kura nyingi chama chao.

Alisema, kwa mwaka huu wanaccm wa Mkoa wa kusini Pemba, wamekusudia kuonyesha maajabu kwa vyama vyengine, huku akiomba amani na utulivu kuendelea.

 Mwisho

MWISHO.