Dk. Mwinyi akiwa rais kuipaisha Zanzibar kimichezo

 

IMEANDIKWA NA HAJI NASSOR, PEMBA  

MGOMBEA wa nafasi ya urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema kama atapata ridhaa ya kushika nafasi hiyo, ataangalia uwezekano mkubwa kuona Zanzibar inakuwa na sheria na kanuni zilizorafiki na michezo.

Mgombea huyo wa urais, aliyasema hayo nje kidogo ya mji wa Chake Chake kisiwani Pemba ikiwa ni sehemu ya ziara yake kisiwani humo, ya kukutana na wananchi na makundi tofauto, wakayi akizungumza na viongozi na wadau wa vyama vya michezo.

Dk. Mwingo alisema maendeleo katika michezo itakuwa mbele Zanzibar mara akiingia madaerakani kwa kule kuzifanyia marekebisho sheria na kanuni ili ziendane na wakati ulioyopo.

Alisema bado sheria na kanuni za michezo haziko rafiki na michezo yenyewe na kusababisha kudamaza michezo ingawa hiulo litakuwa mwisho mwaka huu, mara akipata ridhaa ya kuwa rais wa Zanzibar.

Katika kuleta mageuzi makubwa ya maendeleo ya michezo Zanzibar, alisema ni lazima kuzingatia mambo makuu matatu ambayo ni kuzifanyia marekebisho sera na sheria za michezo.

Alisema lazima makampuni na wafanyabishara wakubwa wachangie kudhamini michezo kwa lengo la kuimarisha michezo mbali mbali Zanzibar kama baadhi ya nchi wanavyofanya.

“Pamoja na kuwaahidi kuwa sera na sheria nitazifanyia marekebisho, laki ni hata wafanyabiashara wakubwa wanayo nafasi nao kutoa mchango wake,’’alisema Mgombea huyo.

Aidha Mgombea huyo wa urais wa Zanzibar kupitia CCM Dk. Hussein Ali Mwinyi, alisisitiza haja kuwa lazima michezo iwezeshwe kwa serikali kuweka fungu kubwa na maalum kwa ajili ya sekta micho.

Hata hivyo Mgombea huyo alisema licha ya kuwepo na kanuni na sheria zinazokataza serikali kutoingilia mambo ya ndani ya michezo, lakini alisema hilo akiwa rais halitomzuia kupiga vita rushwa kwenye michezo.

“Naelewa kuwa sumu kubwa ya kutofika mbali kwenye michezo ni kuwepo rushwa, lakini hili sitolivumilia hata kidogo, maana halitupeleki mbele kimichezo,’’aliahidi Mgombea huyo.

 Kuhusu ligi kuu ya Zanzibar ya soka, Dk. Mwinyi alisema ni aibu kubwa ligi hiyo kukosa wadhamini wakati wapo wadau wengi wenye uwezo wa kudhamini ligi hiyo.

“Mkinichagua kuwa rais aibu hii nitaondoa na kuona ligi yetu inakuwa na hadhi ya aina ya pekee, ili kuona michezo inazaa ajira kwa vijana wetu,’’alieleza.

Mapema Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Zanzibar Dk. Abdulla Juma Mabodi, alisema chama hicho daimi kimeendelea kuwa karibu na makundi yote ya kijamii bila ya ubaguzi.

Mbodi alieleza kuwa, anaamini kuwa suala la michezo halina chama, kwani linagusa maisha ya kila mwananchi duniani kote na sio Zanzibar pekee, ndio maana lazima wanamichezo wapime sera za chama hicho.

Makamu wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar Salum Ubwa, alisema mchezo wa soka ni sehemu kubwa na ya kipekee ya ajira kwa vijana wa Zanzibar kama mazingira bora yakiwekwa.

Kwa upande wake Seif Mohamed Seif akitokea chama cha mpira wa miguu Zanzibar (ZFF) alimuomba Mgombea huyo wa urais wa Zanzibar akumbuke kukutana na wana michezo wa Unguja na Pemba kila wakati.

                         Mwisho