Habari za hivi punde: Ajinyonga akituhumiwa kwa ubakaji Pemba

Habari zilizopatikana kutoka kijiji kimoja cha wilaya ya Chakechake Mkoa wa kusini Pemba, zinaeleza kuwa, kijana mmoja amekutikana chooni akiwa ameshafariki dunia kwa kujinyonga, ambae muda mfupi uliopita inasemekana alishatuhumiwa kwa ubakaji na kuamua kuchukua uamuzi huo.

Tayari madaktari wa hospitali ya Chakechake wameshaufanyia uchunguuzi mwili wa marehemu huyo na taratibu nyingine zimeshakamilika na wameshaukabidhi  mwili wa marehemu kwa ndugu na jamaa zake, kwa ajili ya mazishi.

Seheha wa shehia husika, ameiambia Pembatoday loe Januari 2, mwaka 2020 majira ya 11:00 jioni kuwa kwa sasa hawezi kuzungumza lolote, maana wako njiani wanakwenda mavani kwa ajili ya mazishi ya kijana huyo.

Ili uwe wa kwanza kupata habari za ukweli na uhakika ikiwemo hii, endelea kutufuatilia hatua kwa hatua, huku ukiperuzi kwenye google www.pembatoda.com———- MAANA sisi kukuhabarisha ni fahari yetu.