Habari za hivi punde: Kijana wa Tumbe Pemba aibeba gari

 

Habari zilizonaswa na www.pembatoday.com muda huu wa majira ya 5: 55 mchana wa leo August 3, mwaka 2019, kutoka Vuma wimbi wilaya ya Micheweni mkoa wa kaskazini Pemba, zinaeleza kuwa kijana Ali Khamis Abdalla mkaazi wa Tumbe wilayani humo, ndie mshinde aliejinyakulia gari ndogo.

Msukuma pedeli huyo kabla ya kujifafariji kwa gari hiyo, alikimbia kwa baiskeli yake na wenzake zaidi ya 20, urefu wa kilomita 57, yaani kutoka Chokocho Mkoani mkoa wa kusini Pemba hadi eneo la Ngezi karibu na Makangale, na kisha kuiwacha baiskeli na kukimbia kwa miguu kilomita 11 hadi fukwe ya Vuma wimbi……

je unahitaji habari zaidi na Tamasha la Utalii linaloendelea kisiwani Pemba endelea kufuatilia www.pembatoday.com…….maana kukuhabarisha ni fahari yetu…..