Habari za hivi punde: Mahakama yampa dhamana Babu aliembaka mjukuu wake Wawi

 

TAARIFA za uhakika, zilizonaswa na www.pembatoday.com kutoka viunga vya Mahkama kuu Zanzibar, ilioketi Pemba juzi Januari 31 mwaka huu, zinaeleza kuwa, baada ya mahkama hiyo kumpa dhamana aliekuwa Boss wa Shirika la Taifa la Biashara Zanzibar ‘ZSTC’ wilaya ya Mkoani, Seif Suleiman Kassim anaekabiliwa na tuhuma za ubakaji wa mwanafunzi, mtuhumiwa mwengine nae amepewa dhamana.

Safari hii, aliepewa dhamana ni Babu Ridhiwan Khamis Juma  wa Wawi wilaya ya Chake Chake, anaekabiliwa na tuhma za kumbaka mjukuu wake, ambapo sasa anahemea uraiani, baada ya kuyatimiza masharti yaliowekwa mahakamani, na sasa ataruri tena mahakamani hapo Febuari 5, mwaka huu, kuendelea na kesi yake.

Ni zipi sababu na mazingira yaliomtoa rumande mtuhumiwa huyo, endelea kutufuatilia sisi www.pembatoday.com maana kukuhabarisha ni fahari yetu