Habari za hivi punde: Mtoto mchanga aokotwa Pemba

 

Kama ilivyokuwa mwezi August mwaka jana, ambapo aliokotwa mtoto mchanga aliyetupwa kichakani na mama yake muda mfupi baada ya kujifungua eneo la Pujini wilaya ya Mkoani, na jana tena Machi 25, mwaka huu majira ya saa 12:30 asubuhi, aliokotwa mtoto mwengine akiwa ametupwa na mama yake.

Mtoto huyo alikutikana pembezoni mwa Jangwa la maji ya bahari eneo la Jombwe  Mwambe jimbo Kiwani wilaya ya Mkoani Pemba, na kijana mmoja aliyekuwa kwenye shughuli zake uvuvi baada ya kusikia sauti mtoto huyo akilia.

je kwa sasa mtoto huyo yuko wapi, na mama yake ana akili timamu, na huyo ni mtoto wangapi kumzaa, endelea kufuatilia www.pembatoday.com kupata habari za uhakika. Maana sisi kukuhabarisha ni fahari yetu.