Habari za hivi punde: Wizi wa genereta hospitali ya Chake Chake ZAECA waanza kuwahoji wafanyakazi

 

IKIWA ni miezi miwili na nusu tokea Mamlaka ya Kuzuiarushwa na Uhujumu wa Uchumi Zanzibar ZAECA, kisiwani Pemba, kumnasa daktari akiomba rushwa ya ngono kwa mama mjamzito ndani ya Hospitali ya Chake Chake, safari hii imeshabaini uwepo wa tuhuma za wizi wa genereta lililokuwepo kwa kusambaazia umeme wa dhararu kwenye chumba cha upasuaji na kile cha kuzalishahia hospitalini hapo.

Taarifa zilizonaswa na www.pembatoday.com kutoka ofisi za ZAECA Pemba na kututhibitishwa na Mdhamini wake, zinaeleza kuwa, kufuatia tuhuma hizo, tayari wameshaanza kuwahoji baadhi ya wafanyakazi, ili kumjua muhisika wa tukio hilo pamoja na lile la kuibiwa kwa TV 4 zilizokuwa kwenye sehemu tofauti hospitalini hapo.

Ili uwe wa mwanzo kupata habari za ukweli na uhakika, basi endelea kututembelea sisi www.pembatoday.com MAANA sisi kukuhabarisha ni fahari yetu……..