Habari zilizotufikia hivi Punde, mtu mmoja akatwa miguu ,Pujini Pemba.

Mwanaume mmoja  ambae hajatambulika jina lake, amekutwa akiwa amekatwa miguu yote miwili huku akiugua maumivu makali aliyokua nayo.

Tukio hilo limetokea leo majira ya saa mbili usiku huko Pujini Dodo, wilaya ya chakechake , mkoa wa kusini Pemba.

Chanzo cha habari kimeiarufu PembaToday kuwa , mtu mmoja alikua akitembea barabarani na ndipo alipomuona mtu huyo akiugua kwa maumivu makali huku akiwa amejeruhiwa vibaya.

Taarifa zinasema mtu huyo alishindwa kujizuia na kuanza kupiga mayowe,  akiashiria tukio aliloliona.

” inavyoonekana  huyu mtu amekatwa kwa  mapanga, maana miguu yote miwili imetenganishwa na  miwili  wake” kilisema chanzo hicho

Hadi tunachapisha taarifa hii, mtu  huyo yupo  hospitali ya Chakechake  lakini pia kuna maandalizi ya   kupelekwa hospitali ya Abdallah Mzee Mkoani kwaajili ya matibabu zaidi.

Mpaka sasa Mtuhumiwa (Watuhumiwa) wa tukio hilo bado hawajajuulikana.

Kwa habari kamili kuhusu tukio hili usikose kufuatilia mtandao huu , tutakujuza zaidi, wanahabari wetu wapo makini katika kazi na sasa wanaendelea kukusanya taarifa ili baadae tukujuze kiundani.