Hatua 10 za kumlinda mwanao dhidi ya vitendo vya udhalilishaji kingono

Imewekwa na Salmin Juma – Zanzibar

Email: salminjsalmin@gmail.com

Siku hizi kumezuka tabia mbaya ambazo watoto wadogo wanafanyiwa udhalilishaji wa kingono, hata kulawitiwa , tukiwamurika walimu wa skuli  na wamadrasa ambao wanashutumiwa kudhalilisha kingono wanafunzi,

Hivyo kufuatia matukio hayo na matukio mengine ambayo bado hajavumbuliwa katika vyombo vya habari kumekuwa na wimbi kubwa la watoto wa kike na kiume kudumbukia katika tabia hizo zilizo kinyume na maadili.

Mzazi chukua hatua zifuatazo ni njia 12 unazoweza kutumia kumkinga mtoto wako dhidi ya kupinga tabia hizo.

  1. Zungumza na mtoto wako akueleze juu ya siku yake na mfanye awe rafiki yako ili awe huru kukueleza mambo yake yote mazuri na mabaya, hii itakusaidia kumshauri juu ya mambo mazuri anayotakiwa kufanya na kumkataza juu ya mambo mabaya.
  2. Fahamu muda wake mwingi anatumia na watu wa namna gani.
  3. Mwambie mwanao juu ya vitendo vya udhalilishaji, mwambie mwanao usiruhusu mtu yeyote ashike maeneo fulani ya mwili wake, na akupe taarifa endapo atatokea mtu anamlazamisha kufanya vitendo hivyo.
  4. Chukua hatua fulani ukihisi juu ya vitendo vya udhalilishaji vimefanyika kwa mwanao, aidha kwa kumpeleka hospitali kwa ajili ya uchunguzi wa kina.
  5. Mfundishe mwanao ajue tabia mbaya na nzuri.
  6. Mfundishe mtoto kukataa kufanya kitu ambacho anahisi yeye hakipo sawa.
  7. Mfundishe mtoto juu ya maumbile yake ya siri na kumshauri kuwa chochote kinachofunikwa na nguo za ndani hakitakiwi kushikwa au kuonwa na mtu yeyote.
  8. Mfundishe mtoto kutokukuficha jambo lolote ”asiwe msiri kwako” awe muwazi na mkweli juu ya mambo yote.
  9. Kuwa makini na watu anaokuwa nao muda mwingi, hata hivyo asilimia 80 ya watu wanaofanya udhalilishaji ni wale watu wa karibu na mtoto wako na sio watu asio wafahamu.
  10. Mfundishe mtoto kutoa taarifa pale anapofanyiwa kitu chochote asichofurahishwa nacho.

chanzo:http://dar24.com/hatua-10-za-kumlinda-mwanao-dhidi-ya-vitendo-vya-udhalilishaji-kingono/