Hii hapa nchi ya Afrika ilioanzisha huduma bure ya vipimo vya saratani

 

“Gharama zilikuwa juu sana . Wakati hali hii iliponianza,hivyo ilinibidi niuze kila kitu nlichomiliki,” alisema mgonjwa wa saratani Awa Florence.

“Sina nilichobaki nacho sasa.Mimi ni mjane na sina namna ya kupata fedha ya kufanya vipimo vingine vya kansa.”

Raia huyo wa Senegal anayeishi katika mji mkuu wa Dakar, ambaye alipata saratani ya shingo ya kizazi mwaka jana.

Saratani ni tatizo ambalo linakuwa kubwa barani Afrika na Senegal ni miongoni mwa nchi ambazo haziko nyuma katika kujaribu kuboresha huduma za wagonjwa saratani katika hospitali za umma.

Serikali ya taifa hilo inasema kuwa dawa zitatolewa bure kwa wagonjwa wa wanaosumbuliwa na saratani ya shingo ya kizazi na saratani ya matiti na mpaka asilimia sitini ya magonjwa mengine ya saratani.

Baadhi yadawa muhimu zinahitajika ili kutibu madhara ambayo yanapatikana katika mionzi ya kipimo cha ‘chemotherapy’ , Khady Mbaye Sylla, mkurugeni wa hospitali ya umma aliiambia BBC.

Ni sawa na gurudumu jipya

Lakini pia ugonjwa wa saratani huwa unahitaji tiba nyingine zaidi na sio ya mionzi peke yake, na hiyo huwa inagharimu fedha nyingi ambazo mgonjwa anapaswa kulipa.

“Ni sawa na kupata gurudumu jipya la gari ili gari lako liweze kutembea, unapaswa kununua gesi, uwe na barabara na leseni ya kuendeshea gari lako,” alisema Dkt. Ben Anderson,mkurugenzi wa Mpango wa Afya ya saratani , duniani.

Awa Florence, diagnosed with cervical cancer last year
Image caption“Nilipoona bili yangu ya hospitali kwa mara ya kwanza nilianza kulia tu,”Bi. Florence alisema.

Saratani ya shingo ya kizazi na saratani ya matiti ndio vyanzo vingi vya vifo kwa wanawake wa nchi za kusini mwa jangwa la Sahara, kwa mujibu wa shirika la afya duniani(WHO) .

Ni miaka ya hivi karibuni ambapo kumekuwa na jitihada za kudhibiti na kuzuia magonjwa ya aina hay kuwa jambo linapewa kipaumbele na umma.

Mwaka 2011, shirika la afya duniani WHO lilisema kuwa magonjwa ya muda mrefu ni hatari zaidi katika baadhi ya nchi na husababisha mamilioni ya watu kuwa maskini.

Hivyo hatua ambayo Senegal imefikia inabidi itambuliwe kuwa ni mafanikio makubwa, alisema Dkt. Anderson.

Presentational grey line

Tatizo la saratani nchini Senegal:

  • Saratani ambayo inaongoza ni saratani ya kizazi kwa asilimia 17.8, saratani ya matiti ni asilimia 16.7 , saratani ya ini ikiwa ni 10.2%; ya kibofu 9.1%; na saratani ya tumbo ni 5.2%.
  • Idadi ya watu waliojiandikisha kuwa na kansa kwa mwaka 2018 walikuwa 10,549 -katika jumla ya idadi ya watu milioni 16.
  • Idadi ya vifo vilivyotokana na vifo vya saratani kwa mwaka 2018 ni 7,571

Chanzo: WHO

Presentational grey line

Mpaka hivi karibuni, huduma ya afya kwa wanawake wa Afrika imewekwa kuwa jambo la msingi kwa kuzingatia magonjwa ya kuambukiza na shida wanazozipata wanawake wakati wa ujauzito.

Lakini kuongezeka kwa miaka ya kuishi na vilevile madaktari kueleza hatari za kiafya – zinazotokana na mlo mbaya, kukosa mazoezi, kunywa pombe na sigara kumefanya tatizo la saratani kukua duniani.

Mmoja wa madaktari wachache wa saratani mjini Dakar ameiambia BBC kuwa jitihada zaidi zinahitajika kufanyika ili kupunguza vifo vinavyotokana na saratani.

“Tunahitaji kuapata tiba ambayo inaweza kutibu tatizo hili katika hatua za awali,” alisema Dkt Mamadou Diop.

Pamoja na kuepo kwa mionzi ya chemotherapy, wagonjwa mara nyingi huwa wanahitaji kufanyiwa upasuaji na kupewa tiba mbalimbali.

The scans which showed that Ms Florence has cancer
Image captionHii ni picha inayoonyesha kuwa bi.Florence ana saratani

Nchini Senegal, vipimo vya ‘radiotherapy’ vinagharimu kiasi cha dola 250 na upasuaji ni dola 330.

Hii ni baada ya mgonjwa kufanyiwa vipimo kadhaa ambavyo vinaweza kumgharimu mpaka dola 1600.

Kwa wanawake kama bi.Floence, ambaye anapata kipato cha dola 80, gharama hiyo ni kubwa sana.

Bi.Florence anamatumaini kuwa kutachukuliwa hatua nyingine ambazo zitasaidia wanawake wengine kama yeye, pia ameeleza na kutoridhishwa na jitihada zilizopo.

“Wanasema huduma ni bure lakini hawajui kuwa tunapaswa kujaza fomu na kununua dawa…,” alisema.

” Je, serikali italipia kipimo cha ‘radiotherapy’ kinachogharimu dola 250 au vipimo vya picha vinavyogharimu dola 130? kama serikali italipia vyote hivyo basi sawa- hilo litakuwa jambo zuri sana.”

Uhaba wa Takwimu

A day of free cancer screening organised by Senegal’s anti-cancer league (LISCA) in Dakar
Image captionHuduma ya bure ya vipimo vya kansa

Pamoja na serikali kutangaza kutoa huduma ya vipimo, Dkt Diop anaamini kuwa bado kuna wagonjwa wengi nchini humo hawajaanza kupata huduma yeyote au watu wengi kutokujua kama wana saraani.

Kwa miaka mitano, tatizo limeoneka kupungua kwa utofauti upatao asilimia 10 mpaka 20 katika nchi zinazoendelea, huku nchi tajiri utofauti wake ni asilimia 80 na 90, alisema Dkt Prebo Barango kutoka WHO.

Vigezo vikiwa:

  • Uhaba wa taarifa kuhusu dalili za awali za saratani
  • Tiba kuchelewa na kutopaatikana kwa tiba
  • Huduma duni
  • Umbali wa huduma za afya
  • Gharama za matibabu
  • Mifumo mibovu ya afya

(Chanzo: WHO)

Changamoto kubwa katika mataifa ya Afrika, ni ukosefu wa takwimu haswa tukija kwenye jambo la saratani.

Hali hii inafanya sera kushindwa kuwekwa na kufanyiwa kazi kulingana na tatizo lililopo.

Dr Barango anasema kuwa moja ya tatu ya visa vyote vya saratani vingeweza kuzuilika kama hatua za awali za kuzuia zingefanuika.

Hata hivyo mataifa mengi ya Afrika tayari yameanza kuchukua jitihada za kutoa tahadhari kwa vitu ambavyo vinaweza kuwa visababishi vya saratani, kwa mfano kuwa na vipindi vya kueleza madhara ya tumbaku.

Mataifa mengi ya Afrika kama Botswana, South Africa, Zimbabwe, Senegal, Ethiopia and Malawi na mengineyo – yameanzisha vipimo vya chanjo ya HPV ili kuzuia kansa ya shingo ya kizazi.

Wataalamu wanasema kuwa fedha nyingi zitumike kuelewesha watu kuhusu dalili za awali za saratani na namna wanapaswa kuishi kwa kuzingatia afya zao. (bbc)