Je unaweza kupata virusi vya Corona mara mbili?

 

Baadhi ya wagonjwa wamepona virusi vya Covid-19, baada ya vipimuo kuonesha kuwa hawana coronavirus, lakini je wanaweza kupatikana na virusi vya Covid-19 baadae?.

Maambukizi ya coronavirus, ambayo yanadalili kama ya mafua ya kawaida, kwa kawaida husababisha mgonjwa kuwa na kinga ya mwili.Je kuna tofauti na virusi hivi?

Mwanaume wa miaka 70 na zaidi ni mfano wa awali wa wagonjwa waliowapa madaktari uvumbuzi uliowatia hofu.

Alikuwa ametengwa katika chumba cha hospitali mwezi wa Februari baada ya kubainika kuwa na coronavirus.

Kwa mujibu wa Shirika la habari la Japan NHK, alipona na kurejea katika maisha yake ya kawaida, hata akatumia usafiri wa umma.

Lakini baada ya siku kadhaa akaugua tena na alikua na joto la juu la mwili.

Mwanaume huyo alirejea hospitalini na ilichomshangaza daktari,pale baada ya kufaniwa vipimo alibaini kuwa alikuwa na virusi vya corona tena.

Boris Johnson addresses questions about coronavirus in a press briefingHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionKatika mkakati wake wa kukabiliana na Covid-19 serikali ya Uingereza imezingatia dhana ya kutafuta mbinu za kuimarisha kinga ya mwili kwa umma

Ingawa sio kisa pekee cha aina hiyo kilichopatikana nchini Japan, kwa sasa maambukizi yanayojirudia miongoni hutokea katika watu wachache, lakini ni visa muhimu. Lakini ni kwanini?

Kurejea tena kwa virusi baada ya kupona

Luis Enjuanes, mtaalamu bingwa wa virusi katika kituo cha taifa cha Uhispania cha teknolojia ya vimelea (CSIC), ameiambia BBC kuwa takriban 14% ya wagonjwa ambao hawajapatikana na Covid-19 baada ya kupimwa, baadae wanapopimwa tena hupatikana maambukizi ya coronavirus.

Anaamini haya sio maambukizi ya kwanza, bali ni kisa cha virusi “kurejea tana”.

“Maelezo yangu, miongoni mwa mengine mengi, ni kwamba kwa ujumla hii coronavirus inatengeneza kinga ya umma, lakini kinga hiyo sio thabiti kwa baadhi ya watu binafsi ,” Enjuanes anasema.

“Wakati kinga ya mwili inaposhindwa kuwa ya kutosha, baadhi ya virusi, ambavyo vinasalia katika hifadhi mwilini, huwa vinarejea.”

Virusi vinaweza kuishi katika mwili

Baadhi ya virusi vinaweza kuendelea kuishi ndani ya mwili kwa miezi mitatu au hata zaidi.

Person being tested for Covid-19Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionKwa mujibu wa wataalamu 14% ya wagonjwa waliopata vipimo hasi vya Covid-19 baadae vipimo vyao vilikua chanya later tested positive

“Wakati mtu anapopatikana na virusi halafu baadae anapatikana kuwa hana baadae, dhana ni kwamba ametengeneza kinga ya mwili, kwa hiyo virusi havipaswi kujitokeza tena, kama ilivyo kwa vimelea vingine ,”anasema Enjuanes.

“Lakini baadhi ya virusi vya maambukizi vinaweza kuwa vipo ndani ya nyma za mwili ambazo hazijafikiwa na kinga ya mwili, sawa na sehemu nyingine za mwili.”

Lakini kuna kitu fulani kuhusu ugonjwa wa Covid-19 ambacho kinaendelea kuwashangaza wanasayansi ni: kipindi kifupi baina ya pale mgonjwa anapatwa na virusi tena na baada ya kupona.

Taarifa zaidi kuhusu coronavirus

Unaweza pia kusoma:

Kitu ambacho wanasayansi wameshindwa kukielewa

Tunafahamu kuwa kinga ya mwili inafanya kazi tofauti kwa kila ugonjwa tofauti.

Katika ugonjwa wa surua (ukambi), chanjo moja kama mtoto kwa kawaida hua inatosha kumpatia mtu kinga ya mwili katika kipindi cha maisha yake.

Hata hivyo baadhi ya maafisa wa afya wamependekeza kwambawatu wenye umri filani wanaweza kuwa salama iwapo watarudia kupewa chanjo moja zaidi ya kisasa kuliko wanapochanjwa chanjo ya awali.

Lakini je kuna haja ya kutumia barakoa?

Kuna virusi vingine dhidi ambavyo huifanya chanjo kutokua na ufanisi, kwa hiyo tunahitaji kuongezea nguvu dozi zetu mara kwa mara kwa kipindi fulani.

Na kuna chanjo nyingine, kwa mfano chanjo dhidi ya mafua yanayosababishwa na virusi vinavyoshambulia mfumo wa kupumua (influenza) au mafua ya kawaida, ambazo zinahitaji kuwa zinatolewa kwa watu kila mwaka, kwasababu virusi vyake huwa vina tabia ya kujibadilisha katika hali na umbo jingine.

Bado wanajaribu kuvielewa

Lakini kwasababu Covid-19 ni virusi vipya wanasayansi bado wanajaribu kuelewa kile kinachosababisha kuwepo kwa muda mfupi baina ya maambukizi mawili. (yanayotokea mata ya kwanza na yanayotokea baada ya mtu kupona)

Isidoro Martínez, mtafiti katika taasisi ya Afya ya Madrid – Carlos III Health Institute, mjini Madrid, anasema kwamba ingawa maambukizi ya coronavirus yanayorejea yanaweza kutokea, kinachoshagaza ni kwamba Covid-19 hutokea haraka sanabaada ya mtu kupimwa na kupatikana hana virusi.

A health worker sprays a train station in SpainHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionKinachoshagaza ni kwamba Covid-19 hutokea haraka sanabaada ya mtu kupimwa na kupatikana hana virusi.

“Kama hakuna kinga ya kudumu, katika milipuko ijayo, katika kipindi cha mwaka mmoja au miaka miwili, utapata maambukizi tena. Hilo ni jambo la kawaida,” Martínez aliiambia BBC.

“Lakini ni nadra kwa mtu kupata tena maambukizi ya virusi sawa na aliyopona baada ya kupona . Na pia kulingana na kile tunachokielewa, hii coronavirus haibadiliki kama ilivyo kwa virusi ya mafua,” aliongeza.

Maelezo yake ni sawa na yale aliyoyatoa Enjuanes’.

“Huenda kile kinachotokea ni kwamba watu waliopatikana na Covid-19 tena baada ya kupata vipimo hasi wanakabiliwa na kuongezeka kwa makali ya maambukizi kabla ya virusi kuangamaziwa kabisa”

Coronavirus: Habari njema ni kwamba…

Watafiti wote wawili wanatahadharisha wamba utafiti zaidi unahitajika ili kuelezwa Covid-19.

Shirika la Marekani la Afya-The Pan American Health Organization (PAHO) liliambia BBC kuwa “hii (Covid-19)ni virusi vipya ambavyo tunajifunza kuvielea zaidi kila siku “, kwa hiyo haiwezekani kuelezea visa vya maambukizi baada ya mtu kupona kwa uhakika.

Lakini sayansi inajaribu kupata jibu ili kuzisaidia serikali kuamua ni zipi hatua za umma zinazopaswa kuzichukua. (bbc)