Kifo cha kwanza cha Corana chathibitishwa Ufaransa

 

Mtalii mmoja wa Uchina ameaga dunia Ufaransa baada ya kupata virusi vipya vya Corona na kuthibitishwa kuwa mtu wa kwanza kufa kwa virusi hivyo hayo nje ya Asia.

Mwathirika ni mwanamume, 80, kutoka mji wa Hubei, Uchina kulingana na waziri wa afya wa Ufaransa Agnès Buzyn.

Aliwasili Ufaransa Januari 16 na aliwekwa katika karantini kwenye hospitali moja mjini Paris Januari 25, amesema.

Hadi kufia sasa kumetokea vifo vitatu vya corona nje ya Uchina – Hong Kong Ufilipino na Japani.

Hatahivyo zaidi ya watu 1,500 wameaga dunia kutokana na virusi hivyo ndani ya Uchina vingi vikitokea mji wa Hubei.

Visa vingine 2,641 vimethibitihswa kama maambukizi na kupelekea idadi ya watu waliopata virusi hivyo kufikia 66,492.

Ufaransa ilikuwa imethibitisha visa vya ugonjwa huo 11, ambao kwa sasa unatambulika rasmi kama Covid-19. Watu sita bado wako hospitalini.

Binti ya aliye fariki ni miongoni mwa walioambukizwa, Bi Buzyn amesema hivyo lakini ikasemekana kwamba anaendelea kupata nafuu.

Kando na Uchina bara, zaidi ya visa 500 vimeripotiwa katika nchi 24.

Map showing coronavirus cases outside China
Image captionRamani inayoonesha nchi ambazo zimethibitisha kuwa na visa vya Corona nje ya Uchina
Presentational white space

Awali, Marekani ilisema kwamba inatuma ndege Japani kuhamisha raia wa Marekani waliokwama katika meli ya Diamond Princess ambayo iko kwenye karantini katika bandari ya Japani.

Kati ya watu 3,700 kwenye meli hiyo, 218 wamethibitishwa kuambukizwa virusi hivyo.

Australia pia ilisema kwamba inafikiria kuchukua raia wake walioko kwenye meli hiyo.

Matukio mengine:

  • Beijing imeagiza kila mmoja anayerejea katika mji huo kuwekwa katika karanti kwa siku 14 ama ataadhibiwa.
  • Wizara ya afya ya Misri imethibitisha kisa cha kwanza cha virusi hivyo barani Afrika Ijumaa. Wizara hiyo imemuelezea mwathirika kama mtalii lakini haikusema ni kutoka nchi gani.
  • Wahudumu sita wa afya wamethibitishwa kufa nchini Uchina. mamlaka ya eneo imekuwa ikijitahidi kutoa vifaa vya kujikinga kama vile barakoa, miwani na suti maalum kwa hospitali za Hubei.     (bbc)