Mikononi mwa Polisi, Juisi ya tende kuichanganya na dawa za nguvu za kiume – Z’bar

Mamlaka ya chakula, dawa na vipodozi Zanzibar ZFDA imewakamata watu wawili ambao ni Hamid Hemed Salum (39) na Saidi Hemed Salum (40) wanaodaiwa kuuza Juisi  ya tende ambayo imechanganywa na dawa za nguvu za kiume iliyopewa jina la “4G kifurushi cha wiki”  huko Fuoni Kiembeni na Mwanakwerekwe magari ya Mawe.

Juisi hiyo inadaiwa kuchanganywa na dawa za VIAGRA ambazo hutumika kuongeza kuvu za kiume pamoja na mchanganyiko wa dawa mengine mbalibali.

Akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la tukio hapo Fuoni Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya chakula, dawa na vipodozi Zanzibar Nassir Ali Buheti alisema, kitendo kilichofanywa na watu hao si cha kibinaadamu kwani, dawa wanazo zichanganya kawaida zinakua na utarabu maalum wa kutolewa na aina ya watu sio kuchanganya na juice ili kuwavutia watu kuwa juice ya tende inaongeza nguvu za kiume.

“lengo ni kuwavutia watu kuongeza nguvu za kiume, kumbe wanachanganya na dawa hizi wanaiita 4G kifurushi cha wiki, pia hana kibali kwa upande wa chakula, na aina ya dawa anazo ziuza zinatakiwa kutolewa kwa cheti maalum” alisema Buheti.

Kwa uapande wao watuhumiwa wa tukio hilo wameonekana kukiri kuchanganya dawa hizo kwa lengo la kuwavutia wateja.

Said Saidi Hemed Salum ambae ni mtuhumiwa alisema dawa hizo wanachukuwa famasi mbalimbali na kuzichanganya katika juisi hiyo ingawa awali aliuliza kwa mamlaka husika kuhusu kuuza dawa hizo akajibiwa kuwa hawana utaratibu wa kuwaruhusu kuuza dawa hizo lakini wauze tu.

Biashara hiyo wameifanya kwa takriban miezi sita  na walikua wakitumia gari aina ya  spacio yenye nambari za usajili Z 164 JQ

Jeshi la Polisi  kituo cha Fuoni linawashikiliwa watuhumiwa hao kwa hatua zaidi za kisheria.