Misri, Ethiopia walumbana kuhusu mto Nile

 

Ethiopia inajenga bwawa kubwa linalojulikana kama Renaissance, ujenzi huo unatarajiwa kumalizika mwakani.

Bwawa hilo linalojengwa Ethiopia linatarajiwa kuwa kituo kikubwa zaidi cha kuzalisha umeme barani Afrika.

Ujenzi huo ulianza mwaka 2011 kaskazini mwa Ethiopia ambapo maji yatakayotumika ni asilimia themanini na tano ya maji yanayotiririka kutoka mto Nile.

Hata hivyo ujenzi huo umesababisha kuwepo kwa mzozo kati ya Misri na Ethiopia , huku Sudan pia ikihusishwa na sasa Marekani inajaribu kutatua mzozo huo.

Presentational grey line

Kwa nini kuna kutokukubaliana katika ujenzi huo?

Misri, ambayo inategemea maji ya mto Nile kwa 80%, ina hofu kuwa bwawa hilo litaathiri mfumo wa usambazaji maji na kuifanya Ethiopia kuwa na mamlaka juu ya usambaaji wa maji ya mto mkubwa Afrika.

Kituo cha kuzalisha umeme hakitatumia maji bali bwawa hilo linalojengwa na Ethiopia litaathiri kwa kiwango kikubwa kasi ya mtiririko wa maji.

Muda mrefu utakaotumika kuweka maji katika bwawa ambalo linaenda kuwa kubwa zaidi ya London, inaweza kuleta matokeo pungufu katika kiwango cha mto.

Ethiopia inataka kuweka mradi huo kwa miaka sita.

“Tuna mpango wa kuanza kujaza bwawa hilo katika msimu ujao wa mvua na tutaanza kuendesha mitambo miwili ya umeme kuanzia mwezi disemba mwaka 2020,” Waziri wa maji nchi Ethiopia, Seleshi Bekeli alisema mwezi septemba.

Licha ya kuwa Misri ilipendekeza kipindi cha miaka 10- hii ikiwa inamaanisha kuwa mto unaweza kuathirika sana katika mfumo wa usambazaji wa maji haswa kwenye hatua za awali.

Mazungumzo kati ya Misri, Sudan na Ethiopia ya namna ya kuendesha mradi huo wa bwawa na haujapiga hatua yoyote kwa miaka minne na sasa Marekani inajaribu kuwapatanisha.

Presentational grey line

Kwa nini Misri imekasirika?

Misri inategemea maji ya mto Nile kwa 85% .

Kihistoria, Misri inategemea kwa kiwango kikubwa cha maji ya mto Nile hivyo kama mfumo wa maji hayo utaathirika basi nchi nzima itaathirika.

Makubaliano ya mwaka 1929 iliwapa Misri na Sudan haki ya maji ya mto wote wa Nile.

Wakati wa ukoloni, Misri ilipewa kura ya turufu dhidi ya mradi wowote utakaoendeshwa katika maji hayo kuwa na mamlaka ya kuzuia kama utaathiri sehemu ya maji wanayoyapata.

Ethiopia inasema kuwa hakuna haja ya kuendelea kufungwa na makubaliano ya miongo mingi iliyopita na ndio maana ilianza ujenzi wa bwawa hilo mwaka 2011 bila ya kushauriana na Misri.

River Nile promo imageHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMto Nile unasambaza maji katika mji wa Aswan ambao ni maili 570 kutoka kusini mwa mji mkuu wa Cairo

Rais wa Misri Abdul Fattah al-Sisi alinukuliwa mwezi septemba akisema kuwa ushawishi wa kisiasa hauwezi kuathiri mfumo wa mto huo.

Nchi za kaskazini mwa Afrika zinasema kuwa wasiwasi wao upo kwenye ziwa Nasser, ambalo linatengeneza umeme wa Misri.

Vilevile mradi huo wa usafirishaji unaweza kuathiri sekta ya usafirishaji kama kiwango cha maji kitashuka na kuathiri wakulima ambao wanategemea maji hayo katika kilimo cha umwagiliaji.

Kwa nini Ethiopia inataka kuwa na bwawa kubwa kiasi hicho?

Mradi huu mkubwa zaidi wa kuzalisha umeme utakaogharimu dola bilioni nne unategemewa kuzalisha kiwango kikubwa cha umeme barani Afrika.

Mradi huo ukikamilika unatarajiwa kutoa umeme wa nguvu ya ‘megawatts’ 6,000.

Ethiopia inakabiliwa na tatizo la uhaba wa umeme, zaidi ya 65% ya idadi ya watu nchini humo hawajaunganishiwa umeme.

Hivyo mradi huu ukifanikiwa, utawawezesha wananchi wake kupata umeme wa uhakika na kuuza mwingine kwa nchi za jirani.

Ethiopia dam map
Presentational white space

Ethiopia inaona kuwa bwawa hilo ni suala linalohusu taifa husika.

Mradi wa bwawa hautegemei ufadhili kutoka nje bali inategemea maamuzi ya serikali na ufadhili binafsi ili kulipa mradi huo.

Taifa hilo limekosoa jinsi mataifa ya kigeni yanavyoingilia ujenzi huo.

Je, ujenzi huo una mnufaisha nani mwingine?

Sudan, Sudan kusini, Kenya, Djibouti na Eritrea ni mataifa ambayo yanatarajiwa kunufaika na mradi huo wa bwawa.

Ethiopia dam constructionHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionEthiopia inategemea kumaliza ujenzi huo mwaka 2020

Mataifa mengi kati ya haya yana shida ya umeme.

Kwa upande wa Sudan, mradi huu utakuwa na manufaa zaidi kwa kipindi cha mwaka mzima kwa bwawa hilo kuwepo.

Kwa kawaida , taifa hilo lilikabiliwa na tatizo la mafuriko kwa mwezi Agosti na septemba.

Je, mzozo huu unaweza kupelekea mapigano?

Kumekuwa na hofu kuwa mataifa haya yanaweza kuingia katika vita kama watashindwa kupata suluhu ya mzozo wao.

Mwaka 2013, kulikuwa na ripoti za siri zinaoonyesha kuwa wanasiasa wa Misri wanapendekeza kuwepo kwa mapigano dhidi ya Ethiopia ili kupinga ujenzi wa bwawa hilo.

Rais Sisi alinukuliwa pia akisema kuwa Misri itatumia mbinu zote kulinda haki zake katika mto Nile.

Mwezi uliopita waziri mkuu wa Ethiopia aliwaambia wabunge kuwa hakuna nguvu inayoweza kutumika kusitisha ujenzi wa bwawa hilo. (bbc)