Mjue Waziri Mkuu mwenye umri mdogo zaidi duniani

 

Sanna Marin kutoka nchini Finland atakuwa ndiye waziri mkuu mwenye umri mdogo zaidi akiwa na miaka 34.

Waziri huyo wa uchukuzi alichaguliwa na chama chake cha Social Democratic baada ya kiongozi wake, Antti Rinne, kujiuzulu kama Waziri mkuu. Ataapishwa wiki hii.

Ataongoza muungano wa mrengo wa kati-kushoto na vyama vingine vinne, vyote vikiongozwa na wanawake, watatu kati yao wakiwa na chini ya umri wa miaka 35.

Bwana Rinne alijiuzulu baada ya kupoteza uaminifu miongoni mwa wajumbe wa muungano kwa jinsi alivyoushughulikia mzozo wa maandamano ya wahudumu wa posta.

Atakapochukua mamlaka, Bi Marin atakuwa ndiye Waziri mkuu mwenye umri mdogo zaidi duniani aliyepo mamlakani kwa sasa.

Waziri Mkuu wa New Zealand Jacinda Ardern ana umri wa miaka 39, huku waziri Mkuu wa Ukraine Oleksiy Honcharuk, akiwa na umri wa miaka 35.

Atakuwa ni Waziri Mkuu wa tatu wa kike kuhudumu katika taifa hilo lililoko Kaskazini mwa dunia.

Maisha ya awali ya Bi Marin yalikuwa vipi?

Taarifa za vyombo vya habari zinasema kuwa Sanna Marin alikulia katika familia iliyoishi katika nyumba ya kupangisha akiishi pamoja na mama yake na mpenzi wake wa kike.

Aliuambia wavuti wa Menaiset (nchini Finland) mwaka 2015 kwamba kama mtoto alihisi kama ”asiyeonekana”kwasababu hakuweza kuzungumzia wazi juu ya familia yake.

Lakini alisema mama yake amekuwa akimsaidia sana na kumfanya aamini kuwa anaweza kufanya chochote alichokitaka.

Alikuwa ni mtu wa kwanza katika familia yake kusoma Chuo Kikuu.

Bi Marin rose alipanda vyeo haraka katika chama cha Social Democrats, na kuongoza utawala wa jiji la Tampere akiwa na umri wa miaka 27 na kuwa mbunge mwaka 2015.

Amekuwa waziri wa uchukuzi na mawasiliano tangu mwezi Juni mwaka huu na sasa ana mtoto msichana wa miezi 22.

Kiongozi wa chama cha Kati Katri Kulmun na Marin - sura mpya katika siasa za FinlandHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionKiongozi wa chama cha Kati Katri Kulmun na Marin – sura mpya katika siasa za Finland

Wachambuzi wanasema huenda likawa ni jambo ambalo halikutarajiwa kwa Finland sasa ina Waziri Mkuu mwanamke na viongozi wanne wa chama katika muungano tawala ambao ni wanawake, lakini usawa wa jinsia bado ni tatizo na wanawake katika siasa za Finland wamekua nyuma.

Miongo kadhaa iliyopita, watafiti walibaini kuwa vyama vingi vilikua na wanawake wenye umri mdogo katika nyadhifa muhimu, nafasi ya pili au ya tatu katika ngazi zinazochukua maamuzi, Reetta Siukola, meneja wa maendeleo wa kituo cha Habari cha Usawa wa Jinsia aliiambia BBC .

Kumekuwa na mawaziri wakuu wawili wanawake katika karne hii, ingawa wote walihudumu kwa kipindi kifupi.

Ni dhahiri kuwa wanawake, hususan wanawake vijana, wamekuwa wakakamavu katika siasa za Finland, na katika miaka ya hivi karibuni umma umekuwa ukitegemea 40% au zaidi ya wanawake mawaziri katika serikali ya nchi zao.

Hilo lilibadilika mwaka 2015, wakati serikali iliyokuwa na wanaume wengi ya mrengo wa kati -kushoto ya Juha Sipila ilipochukua madaraka- ni 36% ya mawaziri wake walikua ni wanawake.

Pamoja na kuongezeka kwa kampeni ya #Vuguvugu la MimiPia la dunia , yaani #MeToo movement worldwide, huu ulikua ni mwamko mkubwa wa utetezi wa usawa wa jinsia uliochochea mjadala mkubwa wa kijamii juu ya usawa wa jinsia, Bi Siukola anasema.

Bi Marin anaweza kuchukua mwelekeo upi?

Kuna uwezekano wa kuwepo kwa mabadiliko makubwa ya sera, kwasababu muungano ulikubaliana juu ya mpango ulipochukua madaraka.

Hatahivyo Bi Marin, aliyeshinda uchaguzi wa Waziri Mkuu kwa kura chache, aliweka wazi kuwa mambo hayatakuwa kama yalivyo sasa.

“Tuna kazi nyingi za kufanya ili kujenga upya uaminifu” aliwaambia waandishi wa habari.

Alipuuzilia mbali maswali juu ya umri wake, akisema : ” Sijawahi kufikiria juu ya umri au jinsia. Ninafikiria sababu iliyonifanya niingie katika siasa na mambo yake ambayo tumeaminiwa kufanya na wapigakura:

Presentational white space

Social Democrats kilionekana kuwa ni chama kikubwa katika uchaguzi uliofanyika mwezi Aprili, na kwa hivyo kinaweza kumteaua Waziri Mkuu ambaye ataongoza serikali ya muungano

Bwana Rinne alijiuzulu baada ya mpango wa kukata malipo kwa ajili ya mamia ya wafanyakazi wa posta kusababisha maamndamamo makubwa, na chama cha mrengo wa Kati kikasema kimekosa imani nae.

Hatahivyo bado ni kiongozi wa Social Democrats.

Wakati huo huo chama cha mrengo wa Kati kilisema kuwa Katri Kulmuni atatajwa kama waziri wa fedha. Kulmuni mwenye umri wa miaka 32- alichukua mamlaka kama kiongozi wake mwezi Septemba.

Viongozi wengine watatu walikuwa ni mawaziri katika serikali ya Bwana Rinne na wanatarajiwa kuendelea katika nyadhfa zao- Kiongozi wa muungano wa mrengo wa kushoto Li Andersson kama waziri wa elimu; Kiongozi wa chama cha kijani Maria Ohisalo kama waziri wa mambo ya ndani; na Anna-Maja Henriksson wa Chama cha Swedish People’s Party kama waziri wa sheria.

Finland kwa sasa inashikilia urais wa Muungano wa Ulaya, na wabunge huenda wakaidhinisha mkuu mpya wa serikali katika mkutano wa EU mjini Brussels, tarehe 12 Disemba. (bbc)