Habari za hivi punde: Mtendaji ZSTC Mkoani apata dhamana tuhuma za ubakaji

 

HABARI za kuaminika kutoka viunga vya mahakama kuu Zanzibar, iliokaa kisiwani Pemba, imekubali na kuridhia ombi la dhamana la mtuhumiwa ambae ni ‘boss’ wa Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar ZSTC wilaya ya Mkoani Pemba Seif Suleiman Kassim.

Mtuhumiwa anaekabiliwa na tuhuma za kumbaka  ndani ya ofisi yake mwanafunzi wa darasa la sita, alikuwa rumande miezi miwili iliopita, ambapo juzi Januari 7 alipatiwa dhamana na mahakama kuu, baada ya kupeleka ombi lake mahakamani hapo.

Endelea kufufuatilia unyayo kwa hatua, ili sasa uwe wa mwanzo kupata habari za kweli na za kina, maana sisi Pembatoday kukuhabarisha ni fahari yetu