Mwalimu akanusha mwanafunzi wake kubakwa akienda skuli Pemba

 

IMEANDIKWA NA HASSAN KHAMIS, PEMBA

MWALIMU wa skuli ya Msingi Chwale, Ahmed Juma ambae ni shahidi wa upande wa utetezi, ameiambia mahakama ya mkoa Wete kuwa, sio sahihi kuwa mwanafunzi wake amebakwa wakati akiwa anakwenda skuli kama hati ya mashtaka ilivyodai.

Alidai kuwa, siku na muda wa tukio mwanafunzi huyo sio kweli kuwa alibakwa akiwa darasani, kwani kipindi hco skuli zilikuwa zimefungwa kikawaida.

Mara baada ya shahidi huyo kutinga kizimbani akisubiri taratibu za mahakama, ndipo Mwendesha mashitaka kutoka ofisi ya mkurugenzi wa Mashitaka, Seif Mohamed Khamis alipodai kuwa, shauri hilo lipo kwa ajili ya utetezi, na jumla ya mashahidi wawili wameitwa.

“Mheshimiwa hakimu shauri hili lipo kwa ajili ya utetezi, hivyo tunaiomba mahakama iwaite mashahidi, ili tuanze kuwasikiliza”, alidai.

Hakimu wa mahakama hiyo Abdalla Yahya Shamhun aliridhia ombi hilo na kutangaaza waitwe mashahidi hao mbele ya Mahakama hiyo na kuzna kutoa ushahidi wao.

Shahidi huyo namba mbili, aliithibitishia mahakama hiyo mwanafunzi aliyedaiwa kubakwa ni mwanafunzi wake,  alikua Ahmed Juma ambae ni mwalimu wa darasa wa ingawa anashangaa kusikia mtoto huyo amebakwa.

Alidaiwa kuwa, siku ambayo yeye akiwa ni mwalimu wa darasa lakini pia muda uliodaiwa mtoto huyo amebakwa alikua na kipindi cha ICT na kisha alikua anasahihisha madaftari ya wanafunzi hao ndani ya darasa na mtoto huyo pia alikuwemo darasani wakai na siku hiyo.

“Muda wa majira yasaa 4:30 asubuhi, nilikuwa na kipindi cha somo la ‘ICT’ na huyo anaedaiwa kubwa alikuwepo darasani, nilihakikisha maana baada ya kuwasomesha nilibaki darasani kwa ajili ya kufanya “Marking” (kusahihisha),”alidai.

Mwalimu huyo pia aliwasilisha Mahakamani hapo daftari la mahudhurio ya wanafunzi ambalo lilionekana ni jipya jambo lililowapa shaka upande wa Mashitaka.

Baada ya shahidi huyo kuwasilisha kilelelzo hicho, aliulizwa mtuhumiwa kuwa iwapo atairuhusu Mahakama ibaki na daftari hilo, ili litumike kama kielezo ingaw alikataa.

“Si vyema buku hili la mahudhurio ya wanafunzi lililoletwa na shahidi wangu libakie mahakamani, maana tulilichukua bila ya kuomba ruhusa kwa mkuu wa skuli,’’aliomba

Hata hivyo baada ya kushawishiwa na mahakama kuliacha buku hilo na kuendelea kusimamia uamuzi, Hakimu huyo alimuonya kuacha tabia ya kutumia nyaraka za serikali “document” bila ya kupata ruhusa kutoka kwa mwajiri.

Shahidi namba mbili ambae ni mama mzazi wa mtuhumiwa, aliiambia mahakama kua siku ya tukio hilo, skuli zilikua zimefungwa na anashangaa kusikia mtoto huyo, alibakwa wakati anaenda skuli.

“Kwa kawaida mtoto wangu (mtuhumiwa) na aliebakwa hawasomi darasa moja, lakini kwa sababu ya ujirani wakienda skuli, lazima wafuatane ndio nimeshangaa kusikia amebakwa wakati anaenda skuli, ilhali skuli zilikua zimefungwa,” alidai.

Kesi hiyo  kwa mara ya kwanza ilianza kusikilizwa Mahakamani hapo Machi 9 mwaka huu, na kwa sasa ipo katika hatua ya utetezi.

Baada ya maelezo hayo, hakimu aliiahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 22, mwaka huu kesi hiyo itaendelea na kuomba mashahidi waliobakia waletwa.

Awali ilidaiwa kuwa mtuhumiwa Omar Shehe Faki (27) wa Likoni Wete, anekabiliwa na makosa mawili la kubaka na shambulio la aibu.

Ilidaiwa kuwa, alilitenda kosa hilo Januari 30, mwaka huu majira ya saa 5:00 asubuhi Likoni Wete,  ambao bila ya halali na kwa njia aibu, alimpelekea vidole katika sehemu zake za siri za mbele, mtoto wa miaka 12 na kisha kumbaka jambo ambalo ni kosa kisheria.

Kosa la kubaka ni kinyume na kifungu cha 108 (1) (2) (e) na 109(1) na kosa la shambulio la aibu ni kinyume na kifungu cha 114 (1), cha sheria nambari 6 ya mwaka 2018, sheria ya Zanzibar.

Mwisho