Mwenye ulemavu wa akili na viungo adaiwa kuonja adhabu TAMWA wanena.

Imeandikwa na Salmin Juma – Pemba

Email:salminjsalmin@gmail.com

“Mapambano yanapaswa kuelendelea hadi mwisho wa vitendo hivi vya udhalilishaji, mana hali inaonekana si nzuri” hii ni kauli ya Afisa uwendeshaji (Program Offcer) wa chama cha waandishi wa habari wanawake T’z upande wa Zanzibar afisi ya  Pemba Bi Asha Mussa Omar aliyoitoa wakati  alipokua akizungumza na mwandishi wa habari juu ya tukio la ubakaji linalodaiwa kufanywa na Juma M. Juma wa Makangale Pemba kwa mtoto wa miaka 17 ambae ni mlemavu wa akili na viungo (miguu)

Akizungumza na mwanahabari huyo alisema, wadai katika tukio hilo wasimame kutetea haki yao katika vyombo vya sheria kwani tukio hilo ni baya sana hasa kwakua anaedaiwa kufanyiwa  ni mtoto mlemavu huku akisema kuwa muda mwengine matukio hayo yanashindwa kumalizika kwa sababu adhabu zinazotolewa ni ndogo.

“mfano mtu amembaka mtoto wa miaka 4, utasikia anafungwa miaka 3 au 4, hii ni adhabu ndogo sana, inatakiwa alau afungwe miaka 15 itakua fundisho kubwa kwa wengine” alisema Bi Asha.

Afisa huyo alisema, kamwe TAMWA hawataregeza Kamba katika mapambano dhidi ya vitendo hivyo na watazidi kuwaelimisha wananchi pamoja na maeneo mengine ya kisheria ili alau kuonekane kunatolewa hukumu kubwa kulingana na kosa husika.

Sambamba na kutoa pole kwa familia ya waliyofikwa na mkasa huo, pia amewataka kua tayari kutoa Ushahidi mahakamani ili haki itendeke itakiwavyo..

Nae kamanda wa Polisi mkoa wa kaskazini pemba Shehan Mohd Shehan alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa lilitokea Makangale Wilaya ya Micheweni Pemba, ambapo mtuhumiwa Juma M. Juma mwenye umri wa miaka 25 anatuhumiwa kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka 17 ambae ni ulemavu wa akili na miguu.

“Mtoto huyo alikwenda kumchukua na kwenda kumbaka katika shamba la mipira lililopo Makangale Wilaya ya Micheweni Pemba” alisema.

Kamanda alieleza kuwa, mtuhumiwa amekamatwa na Jeshi la Polisi linaendelea kumuhoji, ambapo watampeleka mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.

Pia alitoa wito kwa wananchi ambao ulnafanana na ule wa afisa ufuatiliaji wa TAMWA wa kuwaripoti wahalifu wa matendo hayo na kuwa mstari wa mbele kutoa ushahidi wakati wanapohitajika kwenda kutoa ushahidi, ili kesi ziweze kupata hatia.