Pata picha kali za matukio kisiwani Pemba

 

SHEHA wa shehia ya Wesha wilaya ya Chake Chake Pemba, Haji Mohamed Ali, akiwaonesha waandishi wa habari wa Pembatoday, hawapo pichani eneo la Rambwe kwenye barabara ya Kijangwani –Birikau, ambapo miaka kadhaa aliwahi kuzama Punda, ambapo kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha kisiwani humo, pamebonyea tena na kukatisha mawasiliano ya barabara baina ya vijiji vya Kijangwani na Tondooni, Kombani na Birikau.

USAFIRISHAJI wa bidhaa kwa kutumia gari ya Ng’ombe bado katika baadhi ya maeneo unaendelea kufanyakazi, kama mpiga picha wa pembatoday, alivyoikuta gari hii eneo la barabara ya Kijangwani- Birikau ikisafafirisha bidhaa hizo.

WANANCHI wanaotumia barabara ya Kijangwani- Birikau wilaya ya Chake Chake, wakishiriki ujenzi wa barabara yao kwa kiwango cha kifusi, baada ya kukatika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha, ambapo serikali ya wilaya ya Chake Chake chini ya Mkuu wa wilaya Rashid Hadid Rashid, ilikubali kuwapelekea gari 10 za kifusi.

MKUU wa Mkoa wa kusini Pemba Hemed Suleiman Abdalla, (kushoto) akipokea msaasa wa mchele, unga wa ngano na sukari kwa ajili ya wananchi wa mkoa wake wanaoishi mazingira magumu, msaada huo umetolewa na Bodi ya Mapato Zanzibar ZRB.

MRATIBU wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania TAMWA Zanzibar kisiwani Pemba Fat-hya Mussa Said akimkabidhi Katib Tawala wilaya ya Chake Chake Omar Juma Ali sabuni maalum kwa ajili ya kunawiya mikono kama kinga ya Corona, ambapo msaada huo umeshaanza kugawiwa kwa wanawake kisiwani Pemba.

MJASIRIAMALI Mayufe Abdalla Rashid kutoka shehia ya Wawi wilaya ya Chake Chake, akionesha sabuni anazotengeneza za maji, ambapo katika hiki cha janga la Corona anasema amepata soko la uhakika, ingawa anaomba dua zoooote janga hilo liondoke leo hii duniani.

HAPA ni eneo la Korosini baina ya kijiji cha Chumbageni na Kidutani, shehia ya Chumbageni Jimbo la Chambani wilaya ya Mkoani Pemba, ambapo kwa sasa eneo la barabara hiyo inatumika nusu, baada ya kuporomoka kuanzia mvua za mwaka 2019 zilizonyesha mwaka huu. Bado mpaka leo Mei 23 hapajajengwa eneo hilo.

HAPA ni eneo la Chake Chake kutokea hospitali kwendea ofisi ya Makamu wa Pili wa rais, na hii gati iliyoumiwa na watawala kwa zaidi ya miaka 70 iliyopita, lakini ndio kwanza iko madhubuti (picha zote kwa hisani ya pembatoday)

‘IKIMALIZIKA hii ntakuwa nachukua abiria kutoka Pemba hadi Unguja’

Duuuuu…….ndio safari kiwanja cha kufurahishia watoto hakifunguliwiiiiii? sawa