Picha: watoto Pemba washerehekea siku yao kwa mtindo mpya

Abuu-bakar Haji, wa Kengeja wilaya ya Mkoani Pemba, akisherehekea siku ya mtoto wa Afrika kwa kutengeneza gari ya mzigo kwa kutumia  rasilimali ya mabipi (majege ya Mgomba), kama alivyokutwa na Pembatoday.

Hawa na watoto wanaosoma chuo cha Qur-an shehia ya Chole wilaya ya Mkoani Pemba, wao wamesherehekea siku yao kwa kupitiliza muda wa masomo chuoni kwao.

Hawa ni watoto wa Chakechake, nao wamepozi

Hawa hapa ni watoto wa Konde, wakiwa safarini, ijapokua sio salama sana.

Kinachokufurahisa nini mtoto wewe Asma

Hawa hapa ni watoto wa Ole, wakimsadiai mjomba wao kumenya viazi vya Chips, kama sio muda wa masomo na wala kazi hii haiwaathiri watoto, hakuna shida.

Hawa hapa ni watoto wa shehia ya Njuguni wilaya ya Micheweni, unajua wanaangalia nini? Wanaangalia wasanii wakiigiza mchezo umuhimu wa kufuata sheria za nchi

Hawa ni wanafunzi kisiwani Pemba, wakisherehekea jambo

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe: Samia Suluhu Hassan, akimjui hali mtoto ambae alilazwa hospitali ya Mkoa wa Abdalla Mzee Mkoani Pemba, wakati alipofanya ziara hospitalini hapo.

 

Kumbuka siku ya mtoto wa Afrika huadhimisha kila ifikapo Juni, 16 ya kila mwaka.

Uongozi, wafanyakazi wote wa Pembatoday tunawatakia watoto wote wa Afrika afya njema na “na sasa iwe basi kuwadhalilisha na kuwafanyia ukatili”

UJUMBE WETU: KWA MWAKA HUU

“Demokrasia ya kweli na utawala bora uanze kwa watoto”