Prof: Lipumba atua Pemba na kupachua bendera katika matawi ya chama.

Imeandikwa na Amina Ahmed – Pemba.

Chama cha wananchi CUF kimesema, kamwe hakitakubali kuona mali za chama hicho zinachukuliwa kinyume na sheria na utaratibu na kikabaki kimya.

Kimesema, kimeandaa mpango maalum wakurudisha matawi yote pamoja na Ofisi zao zilizochukuliwa na chama cha ACT Wazalendo kwa kubadilisha rangi za majengo hayo na kubandika bendera za chama chao kinyume na sheria.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Mwenyekiti msemaji wa kamati maalum ya chama cha wananchi CUF  Nd: Ali Makame Issa alisema, chama hicho kimeandaa matembezi maalumu kwa lengo la kuwajuilisha wananchi kua chama cha CUF bado kipo na kimejipanga kuchukua ofisi zao na kutumika kwa ajili ya harakati za chama kama ilivyokuwa awali

“tumejipanga kurejesha mali za chama chetu zote zilizochukuwaliwa na chama cha ACT Wazalendo” alisema Mwenyekiti huyo.
Baadhi ya wanachama walioshiriki ziara hiyo walisema, hawatokua tayari kupuuza maagizo yatakayotolewa na viongozi wao, kwani wanachotaka kukifanya ni katika hatua za kuimarisha chama.

Ziara maalum ya matembezi ya chama cha wananchi CUF kisiwani Pemba ambayo yamepewa jina la ROUT SHOW ni matembezi yenye lengo la shamrshamra za kumsubiri Mwenyekiti wa chama hicho Pro: Ibrahim Lipumba ambae anatarajiwa kuwa muongozaji wa zoezi la upachuaji bendera za ACT katika matawi yanayodaiwa kuwa ni ya CUF.

Matembezi hayo pamoja na upachuaji wa bendera hizo unatazamiwa kufanyika ndani ya mwezi huu wa 12 katika maeneo mbalimbali kisiwani humo .