Rais mstaafu dk Amani Karume, aona mbali ukuaji uchumi Zanzibar

????????????????????????????????????

 

Rais Mstaafu wa Zanzibar wa awamu ya sita Dk. Amani Abeid Karume alisema kuimarisha huduma ya Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) kutasaidia ukuaji wa uchumi nchini.

Aliyasema hayo alipokuwa akizungumza katika sherehe ya uwekaji wa jiwe la msingi la jengo la Benki ya Malindi ikiwa ni miongoni mwa shamrashamra ya kutimiza miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Alisema kuimarisha huduma za kibenki kwa kutumia njia za kiteknolojia kutawarahisisha wateja kupata huduma zao kwa haraka .

Aidha alisema hatua za Serikali kujenga matawi mbali mbali ya kutoa huduma za kibenki kutasaidia kuepusha msongamano wa wateja pamoja na kuwarahisishia kupata huduma zao kwa haraka .

Alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ilikuwa ikitumia benki hiyo  kwa ajili ya shughuli za kiserikali lakini baada ya kuona benki nyingi zinabinafsishwa ikaanzishwa benki ya watu wa Zanzibar ili  kuwaondoshea usumbuvu wananchi wake.

Aliwataka wafanyakazi wa benki hiyo kuwa makini katika utekelezaji wa kazi zao kwani kufanya hivyo kutasaidia kuepusha migogoro kwa wateja wao .

Hata hivyo aliwataka wateja ambao wanapatiwa mikopo kulipa kwa wakati  na utaratibu uliopangwa ili na wateja wengine waweze kupata kuduma hiyo  .

????????????????????????????????????

Nae Waziri wa Fedha na Mipango Balozi Mohamed  Ramia Abdiwawa amesema ongezeko la kiwango kikubwa cha gawio na kodi ya mapato katika huduma za kibenki kutaimarisha ukuwaji wa uchumi kwa haraka .

Alisema lengo kuu la Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  ni kuwapatia maendeleo wananchi wake na kuwapunguzia makali ya maisha kwa njia ya mikopo .

Mapema Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ), Juma Ameir Hafidh, alisema, kukamilika kwa jengo hilo, kutaweza kukidhi mahitaji ya kibenki kwa wakati wa sasa na baadae.

Aidha alisema kuwa, utayarishaji wa michoro na usimamizi wa ujenzi huo  unafanywa na mshauri elekezi ambae ni kampuni ya NEDCO kutoka Dar-es Salaam.

????????????????????????????????????

Alisema kuwa jengo hilo, litakuwa ni la ghorofa moja (G+M) na lina sehemu mbili ambazo ni sehemu ya jengo jipya na sehemu ya jengo la zamani, ambapo sehemu ya jengo hilo, sehemu ya chini kutakuwa na matawi pacha ya benki ya kawaida na benki ya huduma za kiislamu, na pia kutumiwa na maafisa wote waliopo jengo la darajani na jengo la mpirani.

Alifahamisha kuwa ujenzi huo ulichelewa kutokana na kuchelewa kupatikana kwa mchanga na mawe katika ujenzi, taratibu ndefu za upatikanaji vibali katika kila hatua ya ujenzi katika maeneo ya hifadhi ya mji mkongwe.

Alisema sababu nyengine  ni  tatizo la kuhamisha drainage system ambayo imekata katikati ya jengo, tatizo la kuhamisha umeme ambao umepita chini ya ardhi pamoja na mabadiliko ya jengo ili kuweza kuhudumia baadhi ya wafanyakazi.

Mkurugenzi huyo alisema kuwa  Ujenzi wa jengo hilo, unatarajiwa kumalizika April 2020. (Idara Habari Maelezo Zanzibar)