Tetesi za Soka Ulaya leo Jumatatu 25 /11/ 2019

 

Mchezaji wa Borussia Dortmund Jadon Sancho, 19, anayelengwa na Manchester United anasisistiza kuwa hana mpango wa kuondoka klabu hiyo Januari, japo winga huyo wa England anaonesha ari ya kutaka kuishi Ujerumani licha ya kujiona kama “kisababu” cha kutofanya vyema kwa klabu hiyo. (Athletic via Metro)

Chris Hughton na Rafael Benítez wako katika orodha ya kuchukua majukumu West Ham ikiwa mkufunzi wa klabu hiyo Manuel Pellegrini atafutwa kazi, baada ya kushindwa katika mechi saba. (Guardian).

Meneja mwingine wa Primia League ambaye anakabiliwa na wakati mgumu ni Unai Emery wa Arsenal huku meneja wa Juventus Max Allegri na kocha msaidizi wa Manchester City Mikel Arteta wakitajwa kuwa katika orodha ya watu watakaochukua nafasi yake. (Mail)

Arsenal mara ya mwisho ilishindwa katika mechi sita mtawalio katika mashindano yote mwaka 1998Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionArsenal mara ya mwisho ilishindwa katika mechi sita mtawalio katika mashindano yote mwaka 1998

Kocha wa Napoli, Carlo Ancelotti alihusishwa na tetesi ya kumrithi Mauricio Pochettino katika klabu ya Tottenham, lakini inadaiwa alikuwa “ghali mno” ndio sababu Spurs waliamua kumuakiri Jose Mourinho badala yake. (Mail)

Meneja wa Sheffield United, Chris Wilder pia anapigiwa upatu kuwa mkufunzi wa Hammers baada ya kuongoza klabu hiyo kufikia nafasi ya sita katika jedwali la msimamo wa ligi ya Premia. (Mirror)

West Ham wanajiandaa kumuuza kiungo wa kati wa Colombia Carlos Sanchez,33, mwezi Januari, mchezaji huyo akitarajiwa kuwa bila klabu msimu ujao. (Sun)

Carlos SanchezHaki miliki ya pichaREX FEATURES
Image captionWest Ham wanajiandaa kumuuza kiungo wa kati wa Colombia Carlos Sanchez

Tottenham inamfuatilia mchezaji wa Bournemouth Nathan Ake, 24, huku beki huyo Mdachi akipigiwa upatu kuchukua nafasi ya Jan Vertonghen, ambaye kandarasi yake Spurs inakamilika msimu wa joto wa mwaka 2020. (Football Insider)

Leeds, Aston Villa na Crystal Palace zimeonesha ishara ya kutaka kumsajili mshambuliaji wa Liverpool Rhian Brewster, 19, kwa mkopo ifikapo mwezi Januari. (Star)

Arsenal huenda ikamkosa beki wa kati wa Barcelona Samuel Umtiti, 26, huku kiungo huyo wa Ufaransa ikipania kurejea katika klabu yake ya zamani ya Lyon ikiwa ataamua kuondoka Nou Camp. (L’Equipe – in French)

Samuel UmtitiHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionArsenal huenda ikamkosa beki wa kati wa Barcelona Samuel Umtiti

Beki wa kati na nyuma wa Wolves wa chini ya miaka 23, Owen Otasowie, 18, anatakiwa na mabingwa wa Ligue 1, Paris St-Germain na Schalke ya Bundesliga. (Sun)

Mchezaji wa Bournemouth Ryan Fraser amehusishwa na uhamisho wa kwenda Everton, Liverpool na Arsenal wakati mkataba wake utakapomalizika msimu ujao, lakini winga huyo wamiaka 25 anasisitiza kuwa hajafikia uamuzi wa hatma yake ya siku zijazo. (mirror)

Mazungumzo ya kurefusha mkataba wa mshambuliaji Paris St-Germain Kylian Mbappe yanaendelea,huku rais wa klabu hiyo Leonardo akipatia umuhimu mkubwa hatma ya nyota huyo wa Ufaransa wa miaka 20. (L’Equipe – kwa Kifaransa)

Kylian MbappeHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMazungumzo ya kurefusha mkataba wa mshambuliaji Paris St-Germain Kylian Mbappe yanaendelea

Newcastle United inamfuatilia Monaco beki Benoit Badiashile baada ya wasaka vipaji kumtazama kiungo huyo wa miaka 18-akicheza katika mechi ya klabu yake mjini Bordeaux. (Newcastle Chronicle)

Kiungo wa kati wa Scotland na Aston Villa John McGinn, 25, atasalia Villa Park licha ya tetesi zinazomhusisha na uhaisho wa mwezi Januari. (Star).

Manchester United itapokea £850,000 kutoka kwa Juventus msimu ujao kama mojawapo ya makubaliano ambayo yalimfanya mshambuliaji wa zamani wa United Cristiano Ronaldo, 34, kujiunga na klabu hiyo ya Italia kutoka Real Madrid 2018. (Sun Jumapili)

Christiano Ronaldo aliichezea Man United klabu ya Kuelekja Real madrid

Mkufunzi wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer anaamini hatowasajili wachezaji anaowalenga katika dierisha la uhamisho la mwezi Januari na sasa atalazimika kutafuta uhamisho wa mkopo badala yake. (Sunday Telegraph)

Mshambuliaji wa Manchester City na England Raheem Sterling, 24, hatotia saini kandarasi ya £450,000 kwa wiki hadi pale atakapothibitisha kuwa mkufunzi Pep Guardiola atasalia katika klabu hiyo kwa kipindi cha muda mrefu. (Sun Jumapili)

Raheem SterlingHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMshambuliaji wa Manchester City na England Raheem Sterling, hatotia saini kandarasi mpya wiki hadi pale atakapothibitisha kuwa mkufunzi Pep Guardiola atasalia katika klabu

Man United na Paris St-Germain wako tayari kulipa Pauni 60m (£52m) ili kumnunua kiungo wa kati wa Itali Nicolo Zaniolo, 20. (Il Messaggero – kwa Kitaliano)

Arsenal wanakabiliana na Inter Milan katika kumsaini kinda mshambuliaji wa Flamengo na Brazil mwenye umri wa miaka 17 Reinier Jesus, 17. (Sun on Sunday)

Mshambuliaji wa Inter Milan na Ubelgiji Romelu Lukaku, 26, amesema kwamba alijua kwamba wakati wake katika klabu ya Man United umekamilika wakati mkufunzi Solskjaer alipoanza kumtumia katika wingi . (Football Italia)

Romelu LukakuHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMshambuliaji wa Inter Milan na Ubelgiji Romelu Lukaku, 26, amesema kwamba alijua kwamba wakati wake Man United umekamilika wakati mkufunzi Solskjaer alipoanza kumtumia katika wingi

Mario Balotelli analengwa na klabu ya Galatasaray. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 alijiunga na klabu yake ya nyumbani ya Brescia msimu uliopita. (Calciomercato – in Italian)

Newcastle United itamuuza kiungo wa kati wa South Korea Ki Sung-yueng, 30, in January. (Football Insider) (CHANZO BBC)