Trump akaribishwa kuhudhuria kikao cha tuhuma zinazomkabili au………

 

Bunge la Congress nchini Marekani limemualika rais wa nchi hiyo Donald Trump katika kikao chake kitakachosikiliza tuhumazinazomkabili rais huyo tarehe 4 Disemba.

Jerrold Nadler, mwenyekiti wa chama kamati ya Congress ya masula ya sheria kutoka chama cha Democratic, alisema kuwa Bwana Trump anaweza kuhudhuria au ”akome kulalamika juu ya mchakato” huo.

Kama atahudhuria, rais ataweza kuwahoji mashahidi.

Kikao hicho kitakua ni hatua itakayowezesha kuanzishwa kwa hatua nyingine katika mashtaka , yanayomuhusisha na Ukraine chanzo chake ni simu ambayo rais Trump alimpigia rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky.

Trump anashutumiwa kuwashinikiza viongozi wa Ukraine kumchunguza hasimu wake kisiasa Joe Biden(kulia)Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionTrump anashutumiwa kuwashinikiza viongozi wa Ukraine kumchunguza hasimu wake kisiasa Joe Biden(kulia)

Katika mawasiliano ya simu hiyo Trump alimtaka Bwana Zelensky amchunguze Joe Biden, ambaye kwa sasa ndie mgombea aliye mstari wa mbele kuwania kiti cha urais kwa tiketi ya chama cha Democratic katika uchaguzi wa urais mwaka ujao, na mtoto wake wa kiume Hunter Biden, ambaye awali alifanyia kazi kampuni ya nishati ya Ukraine Burisma.

Uchunguzi unataka kubaini juu ya ikiwa Bwana Trump alitumia tisho la kuzuwia msaada wa jeshi la Marekani kwa Ukraine ili kuifanya imchunguze Biden na mwanae. Rais Trump amekana kufanya kosa lolote na ameutaja uchunguzi kuwa ni ” hila”.

Wiki iliyopita, Kamati ya masuala ya ujasusi ilikamilisha wikimbili za kusikiliza , kufuatia wiki kadhaa za vikao vya faragha ambapo waliwahoji mashahidi.

Adam Schiff, mwenyekiti wa kamati ya ujasusi, anayeongoza uchunguzi huo alisema kamati za masuala ya kigeni na intelijensia – sasa zinaifanyia kazi ripoti yao, ambayo itatolewa tarehe 3 Disemba.

Jerrold Nadler alisema nini ?

Bwana Nadler alisema katika taarifa yake kwamba alikuwa amemuandikia Bwana trump akimualika kuhudhuria kikao cha kusikiliza tuhuma dhidi yake mwezi ujao.

” Rais ana uamuzi wa kuchukua ,” Bwana Nadler alisema “Anaweza kuchukua fursa ya kuwasilishwa katika kikao cha tuhuma au aache kulala juu ya mchakato.

” Natumai kwamba atachagua kushiriki katika uchunguzi, moja kwa moja au kupitia baraza, kama walivyofanya marais wengine kabla yake.”

Jerrold NadlerHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionJerrold Nadler alisema Bwana Trump anafaa kuhudhuria kikao au “akome kulalamika”

Katika barua yake kwa rais, Bwana Nadler alisema itakuwa ni fursa nzuri ya kujadili mashtaka kwa misingi ya kihistoria na kikatiba s

” Pia tutajadili juu ya ikiwa madai ya matendo yako yataliwezesha bunge kutekeleza mamlaka yake ya kuidhinisha vipengele vya mashtaka ,” aliongeza.

He has given Mr Trump until 18:00 EST (23:00 GMT) on 1 December to confirm whether or not he will be at the hearing, and if so, to let the committee know who his counsel will be.

Nini kitakachofuata katika mashtaka ?

Kamati ya masuala ya sheria ya bunge inatarajiwa kuanza kuandika miswada ya tuhuma – ambazo ni mashtaka ya kufanya makosa dhidi ya rais- mapema mwezi Disemba.

Baada ya kura, bunge linalodhibitiwa na Democratic , kesi itaendeshwa katika bunge la seneti linalodhibitiwa na Republican.

Kama Bwana Trump atapatikana na hatia kwa theluthi mbili ya wabunge- matokeo ambayo yanaonekana huenda kutopatikane- atakuwa ni rais wa kwanza wa Marekani kung’olewa madarakani kupitia mashtaka ya aina hii

Ikulu ya White House na baadhi ya Warepublican wanataka kesi iendeshwe kwa wiki mbili tu.

Uchunguzi dhidi ya Trump

Kura ya maoni iliyoendeshwa na shirika la A YouGov ilisema kuwa 55% ya Wamarekani wangeunga mkono kushtakiwa kwa Trump ika ingethibitishwa kwamba Trump alisitisha msaada wa kijeshi kwa ukraine ili kuwashinikiza maafisa wa nchi hiyo kumchunguza Joe Biden. (chanzo BBC)