Vijana kuweni makini musitumike kisiasa.

Vijana nchini wametakiwa kutokutumiwa na wanasiasa kuhatarisha amani kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.
Akizungumza na Pemba today mwenyekiti wa baraza la vijana Zanzibar ndugu, Khamis Rashid Kheir alisema vijana hutumika zaid kuchochea vurugu hasa katika nyakati za uchaguzi.
“niwaambie vijana sisi ndio tunatumika kuchochea vurugu huvyo niwasihi tutumike kwenye mambo ya kuleta maendeleo” alisema ndugu,Khamis
Alisema nimatumaini yake kuwa uchaguzi utakuwa amani na utulivu kutokana na serikali kujiandaa kikamilifu kwa kuimarisha vyombo vya ulinzi na usalama ambapo amevitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuwachukulia hatua viongozi wa kisiasa wanaotoka kauli za kichochezi.
“Nivyouona uchaguzi wa mara hii utakuwa wa amani na utulivu kwani ninauhakika serikali kupitia vyombo vyake vya ulinzi na usalama imejipanga” alisema mwenyekiti huyo
“Pia niiombe Serikali kuwachukulia hatua viongozi wanaotoa kauli za uchochezi na kuhamasisha vurugu” Aliongezea
Akizungumzia suala la ushiriki wa vijana kwenye kinyang’anyiro wa nafasi mbalimbali za uongozi alisema wamejipanga kama vijana kushiriki kwa wingi katika kugombania nafasi mbalimbali za uongozi katika vyama vyote.
“Vijana tumejipanga tuna wenyeviti wa mabaraza ya vijana wilaya kumi na moja anatumai japo wawili katika hao watagombania nafasi yoyote ya uongozi” alisema ndugu, Khamis
Tanzania inatarajia kufanya uchaguzi wa uraisi wajamhuri ya muungano wa Tanzania,uraisi wa Zanzibar,ubunge,uwakilishi na udiwani mwezi oktoba mwaka huu.