Wafahamu waafrika wanaomuombea rais Donald Trump ushindi

 

Licha ya kutoa matamshi ya dharau kuhusu Afrika, Rais wa Marekani Donald Trump amevutia wafuasi waumini wa Kikristo wengine barani.

“Muombeeni [Trump] kwa sababu wakati Mungu anapoweka watoto wake katika nafasi fulani, wakati mwingine jehanamu hufanya kila kitu kumwangamiza mtu huyo,” alisema Mchungaji wa Nigeria Chris Oyakhilome, muhubiri maarufu wa televisheni, mwezi Juni.

Pia alitahadharisha kuwa wakosoaji wa rais wa Republican ambaye anatafuta kuchaguliwa tena mwezi Novemba wanawachukia wafuasi wake.

Wana hasira na Trump kwa kuwaunga mkono Wakristo, lazima mfahamu. Hivyo wanaowachukia kweli ni nyinyi mlio Wakristo,” alisema mchungaji huyo ambaye matangazo yake ni maarufu sana duniani, ikiwemo Marekani.

Rais Trump amekuwa mtu wa kutatanisha ulimwenguni kote lakini ni maarufu katika nchi za Kiafrika kama Nigeria na Kenya, kulingana na utafiti wa Pew uliotolewa mnamo mwezi Januari, ambapo wafuasi hawaonekani kuwa na wasiwasi kuwa kutokana na kuzitaja nchi za Kiafrika kuwa “chafu “mnamo 2018.

Nigeria na Kenya ni nchi zinazofuata mikondo ya kidini . Makanisa ya Mega yanaenea Kusini mwa Nigeria – taifa lenye watu wengi barani Afrika – na nchini Kenya wanasiasa wengi huenda kwenye mahubiri ya kanisa kuhutubia wafuasi wao, huo ndio umaarufu wao.

Makundi mengi ya Kikristo ya Kiinjili barani Afrika, ambayo ni zaidi hupinga kuavya mimba, vitendo vya mapenzi ya jinsia moja na hupinga mkono wa Israel, hayakuwa na nia na mtangulizi wake wa Democrat Barack Obama, licha ya kuwa na mizizi ya Kenya.

“Utawala wa Obama ulikuwa unashinikiza ajenda ya ukombozi hapa Afrika na ajenda hiyo ilikuwa ya wasiwasi kwa baadhi yetu viongozi wa Kikristo. Ilikuwa faraja kwamba wakati wa Trump alikuwa amerudi nyuma kidogo,” Richard Chogo, mchungaji katika Kanisa la Deliverance katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi, liliambia BBC.

Aliusifu utawala wa Trump kwa kuondoa ufadhili kwa baadhi ya mashirika kama vile Marie Stopes, ambayo hutoa huduma za uzazi wa mpango na uavyaji mimba salama katika nchi kadhaa barani Afrika.

Shirika hilo lilikosoa marufuku ya ufadhili wa Marekani wa mwaka 2017, likisema kwamba “inaweka maisha ya wanawake hatarini”.

Lakini Mchungaji Chogo anakubaliana na sheria nchini Kenya ambapo utoaji mimba ni haramu isipokuwa iwapo afya ya mama iko hatarini, akisema kwamba kuhalalisha utoaji mimba ni sehemu ya “ajenda ya kudhibiti idadi ya watu”.

Bwana Trump amejuvuna kwamba amewafanyia mambo mengi mazuri Wamarekani weusi
Bwana Trump amejuvuna kwamba amewafanyia mambo mengi mazuri Wamarekani weusi

Black Lives MatterMjadala kuhusu utoaji mimba umekuwepo katika siasa za nchini Marekani kwa karibu miongo minne.

Wainjilisti weupe wameungana kuhusu suala hilo na kugeuza harakati zao za kupambana na utoaji-mimba kuwa nguvu ya kisiasa yenye ushawishi.

Baada ya uamuzi wa kihistoria wa 1973 Roe v Wade na Mahakama kuu ya Marekani kuhalalisha utoaji mimba, wainjilisti weupe, ambao wakati huo hawakuwa na uhusiano wowote kisiasa na moja ya vyama kuu viwili, walimuunga mkono Ronald Reagan wa Republican katika uchaguzi wa urais wa 1980 dhidi ya kiongozi wa Democratic wa wakati huo Jimmy Carter

Wainjilisti weupe tangu hapo wamekuwa kambi muhimu ya kupiga kura kwa Chama cha Republican na wameongeza ushawishi wao ulimwenguni.

Hii ni licha ya waprotestanti weusi nchini Marekani kuwa wengi wa Democrat na kukosoa rekodi ya Bw Trump, kulingana na utafiti wa hivi karibuni wa Pew, Emeka Ezeji, mchungaji na shemasi mkuu katika Kanisa la Kimishenari la Kianglikana katika jimbo la Enugu Kusini Mashariki mwa Nigeria, anasema maoni yake ya kisiasa yamedhamiriwa tu “na yale maandiko yanasema”.

“Imani ni kitu binafsi, yangu ni ya kuunga mkono maisha … Wakristo wa Kiafrika wanaamini kuwa rais wa Republican ni bora kwa Marekani na ulimwengu,” alisema.

Amekuwa akimuombea Bw Trump kumshinda mgombea wa Chama cha Democrat Joe Biden mwezi Novemba, na kutenga muda kila siku kumwombea rais apone wakati alikuwa hospitalini hivi karibuni baada ya kukutwa na maambukizi ya virusi vya corona.

Kama Mchungaji Chogo, yeye pia anaamini kwamba “udhaifu” wa Bw Trump haupaswi kufunika yaliyo”mazuri ” kwetu.

Kwa mfano, anatupilia mbali harakati za black lives matter(BLM), ambayo Bwana Trump ameitaja kama “ishara ya chuki”, akisema “imetekwa nyara kwa maono yake”. (bbc)