Waombolezaji wakusanyika Baghdad kumuaga jenerali

 

Umati mkubwa watu umekusanyika katika mji mkuu wa Iraq, Baghdad kushiriki maandamano ya mazishi ya kamanda wa jeshi la Iran Qasem Soleimani, aliyeuawa katika shambulio la angani lililotekelezwa na Marekani siku ya Ijumaa.

Soleimani alikuwa kiungo muhimu katika oparesheni ya Iran Mashariki ya kati na taifa hilo limeapa “kulipiza kisasi” mauaji yake.

Mkusanyiko huo wa mjini Baghdad ni mwanzo wa siku kadhaa ya maombolezi ya Soleimani.

 

Makundi ya watu mjini Baghdad ulikuwa hapo kuomboleza kifo cha Abu Mahdi al-Muhandis, mmoja wa kamanda wa Iraq ambaye kundi lake la Kataib Hezbollah linaloungwa mkono na Iran pia aliuawa katika shambulio hilo.

Waandamanaji walianza kukusanyika mjini Baghdad mapema asubuhi ya Jumamosi wakipeperusha bendera ya Iraq naya waasi wakiimba “kifo kwa Amerika”.

Waandamanaji walizunguka bara bara za mji huo wakibeba mababgu yaliyo na picha ya Soleimani huku wengine wakiwa na mabangu yaliyo na picha ya kiongozi mkuu wa kidini wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei.

Waandamanaji wakiziingira gari lililobeba jeneza la Qasem Soleimani,Haki miliki ya pichaAFP
Image captionWaandamanaji wakiziingira gari lililobeba jeneza la Qasem Soleimani

Ripoti zinasema mwili ya raia huyo wa Iran aliyeuawa katika shambulio hilo utasafirishwa nchini humo Jumamosi jioni, ambako siku tatu ya maombolezo imetangazwa kwa heshima ya jenerali.

Mazishi yake yatafanyika siku ya Jumanne nyumbani kwake Kerman eneo la kati laIran.

Baadhi ya raia wa Iran walisherehekea taarifa za kuuawa kwa Soleimani mjini Baghdad.

Alilaumiwa kwa kupanga ghasia na kuunja maandamno ya amani ya kupigania demokrasia katika miezi ya hivi karibuni.

Presentational grey line

Mshambulizi mapya ya angani Iraq

Televisheni ya taifa ya Iraq imetangaza mashambulio mengine ya angani nchini humo saa 24 baada ya kuawa kwa Soleimani.

Vyanzo vya habari vya jeshi nchini Iraq vimeliambia shirika la habari la Reuters kuwa watu sita wameuawa katika shambulio hilo jimpya,ambalo lililenga msafara wa waasi wa Iraq asubuhi ya Jumamosi.

Msemaji wa jeshi la muungano linaloongozwa na Marekani katika eneo hilo amesema hawakuhusika na shambulio hilo.

Marekani imesema kuwa wanajeshi 3,000 wa ziada watapelekwa mashariki ya kati kujibu hatua yoyote ya kulipiza kisasi.

Moja ya magari katika msafara wa Soleimani iiliwaka moto baada ya kushambuliwa katikauwanja wa ndege wa kimataifa mjini BaghdadHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMoja ya magari katika msafara wa Soleimani iiliwaka moto baada ya kushambuliwa katikauwanja wa ndege wa kimataifa mjini Baghdad

Akizungumza na vyombo vya habari katika mgahawa wa Mar-a-Lago mjini Florida, Bw. Trump alisema katika shambulio la siku ya Ijuma: “Jeshi la Marekani katika opareshi stadi ilifanikiwa kumuua gaidi nambari moja duniani, Qassem Soleimani.”

Bw. Trump alisema Soleimani alikuwa “anapanga kushambulia wanadiplomasia na maafisa wa kijeshi wa Marekani lkini tulifanikiwa kupata kabla hajatekeleza mpango wake na kumuangamiza”.

Hata hivyo maafisa wa utawala wa Trump hawakutoa taarifa zaidi kuhusiana na shambulio hilo na kile kilichowafanya kuchukua hatua ya kumuua ghafla Soleimani.

Marais wa zamani wa Marekani Barack Obama na George Bush wamepinga hofu kuwa shambulio dhidi ya jenerali huyo lilikuwa hatari.

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imetoa onyo kwa raia wake baada ya shambulio hilo kuondoka Iraq mara moja kupitia njia yoyote inayowezekana.

Iran imepokeleaje hatua hiyo?

Katika taarifa kufuatia kifo cha Soleimani, kiongozi mkuu wa kidini Ayatollah Ali Khamenei alisema: “Kuelekea kwake kwa Mungu sio mwisho wa mpango wake, kisasi kikali kinawasubiri wahalifu walimwaga damu yake na ya shujaa mwingine Ijuma asubuhi.”

Qasem SoleimaniHaki miliki ya pichaAFP/GETTY
Image captionPentagon ilithibitisha kuwa vikosi vya Marekani vilimuua Jenerali Soleimani

(bbc)